Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda (kulia) akiongoza Viongozi na Watendaji wa Mkoa huo kufanya usafi katika eneo la Soko Kuu la Jiji la Mwanza Mei 30, 2026 wakati wa zoezi la usafi wa mazingira Mkoani humo kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani mwaka 2026.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda (Katikati-traki suti nyekundu) akiongoza viongozi na watendaji Mkoani humo kufanya usafi katika eneo la Soko Kuu la Jiji la Mwanza Mei 30, 2026 wakati wa zoezi la usafi wa mazingira Mkoani humo kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, 2026.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda akiwaonesha Maafisa Mazingira wa Jiji la Mwanza kiasi cha taka ngumu zilizoenea katika eneo la Soko Kuu la Jiji hilo Mei 30, 2026 wakati wa zoezi la usafi katika eneo hilo kuelekea maadhimisho kuelekea Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, 2026.
Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Jiji la Mwanza wakifanya usafi katika eneo la soko hilo wakati wa zoezi la usafi wa mazingira Mkoani humo Mei 30, 2026 ikiwa ni maandalizi kuelekea Kilele cha Maadhimisho Siku ya Mazingira Duniani, 2026.
Watumishi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Sheila Kikula (wa pili kutoka kushoto) na Bw. Lucas Sebida (wa pili kutoka kulia) wakiungana na wafanyabiashara wa Soko Kuu la Jiji la Mwanza Mei 30, 2026 kufanya usafi katika eneo hilo wakati wa zoezi la usafi wa mazingira Mkoani humo ikiwa ni maandalizi kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, 2026.
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Bw. Balandya Elikana (kulia) akiwa na vitendea kazi mbalimbali kwa ajili ya kuanza zoezi la usafi katika eneo la Soko Kuu la Jiji hilo wakati wa zoezi la usafi wa mazingira Mkoani humo Mei 30, 2026 ikiwa ni maandalizi kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, 2026.
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana (kushoto) akiwa na Afisa Utumishi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Sheila Kikula (katikati) wakifanya usafi katika eneo la Soko Kuu la Jiji la Mwanza wakati wa zoezi la usafi wa mazingira Mkoani Mei 30, 2026 ikiwa ni maandalizi kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, 2026
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda (kulia) akiongoza viongozi na watendaji wa Mkoa huo kufanya usafi katika eneo la Soko Kuu la Jiji la Mwanza Mei 30, 2026 katika zoezi la usafi wa mazingira Mkoani humo kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, 2026.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda (wa pili kushoto) akiwa pamoja na Viongozi na Watendaji wa Mkoa huo wakikagua maeneo mbalimbali ya Soko Kuu la Jiji la Mwanza Mei 30, 2026 wakati wa zoezi la usafi wa eneo hilo kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani mwaka 2026. Kulia ni Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana, Bw. Thomas Salala
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda (wa pili kulia) akiwa na viongozi na watendaji mbalimbali wa Mkoa huo wakikagua maeneo mbalimbali ya Soko Kuu la Jiji la Mwanza Mei 30, 2026 wakati wa zoezi la usafi wa katika eneo hilo kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani mwaka 2026. Wa kwanza kulia ni Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana, Bw. Thomas Salala.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda akitoa salamu za Mkoa huo muda mfupi baada ya kukamilika kwa zoezi la usafi katika eneo la Soko Kuu la Jiji la Mwanza Mei 30, 2026 kuelekea maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, 2026. Kushoto ni Afisa Misitu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Lucas Sabida.
Afisa Misitu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Lucas Sabida akitoa salamu za Ofisi hiyo muda mfupi baada ya kukamilika kwa zoezi la usafi katika eneo la Soko Kuu la Jiji la Mwanza Mei 30, 2026 kueleka Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, 2026. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda.
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana, Bw. Thomas Salala akitoa salamu za Wilaya hiyo wakati wa zoezi la usafi katika eneo la Soko Kuu la Jiji la Mwanza Mei 30, 2026 kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani mwaka 2026. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda na kushoto ni Afisa Misitu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Lucas Sabida.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda (kulia) akiwa pamoja na Viongozi na Watendaji wa Mkoa huo wakikagua maeneo mbalimbali ya Soko Kuu la Jiji la Mwanza wakati wa zoezi la usafi wa eneo hilo Mei 30, 2026 kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani mwaka 2026. Katikati ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Amiri Mkalipa.
.....................................................
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda amewataka Maafisa Mazingira kuwachukulia hatua za kisheria wafanyabiashara wanaokiuka Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira kwa kutupa taka ovyo ndani ya mifereji ya maji taka katika Soko Kuu la Jiji hilo.
Mhe. Mtanda ametoa kauli hiyo Mei 30, 2026 wakati alipoongoza viongozi, watendaji na wananchi Mkoa huo katika zoezi la usafi wa mazingira katika eneo la Soko Kuu la Jiji hilo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho kuelekea Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani mwaka 2026.
Amesema baadhi ya wafanyabiashara katika soko hilo wamejenga mazoea ya kutupa taka ovyo katika mifereji ya maji taka katika Soko hilo hali inayochangia kukithiri kwa uchafu na hivyo kuchochea kasi ya uharibifu wa mazingira.
“Natoa maelekezo kwa maafisa mazingira wa jiji na meneja wa soko kuhakikisha kunakuwa na utekelezaji wa Sheria ya Afya na Usafi wa mazingira katika Soko hili na kila anayekiuka sheria hakikisheni anatozwa faini” amesema Mtanda.
Aidha Mhe. Mtanda amesema faini hizo zitakazolipwa na wafanyabiashara hao zitatumika katika kulipa gharama za huduma ya usafi inayotolewa na Halmashauri ya Jiji na hivyo kuhimiza watumiaji wa soko kuzingatia taratibu za usafi ili kulinda mazingira.
Mhe. Mtanda pia amewalekeza maafisa mazingira kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa wafanyabiashara waliopo ndani ya soko ili kuhakikisha wanatekeleza maelekezo, miongozo na ya sheria zilizopo ili huduma za soko hilo ziendelee kuwa endelevu kwa wananchi.
Amesema suala la usafi ni ustaarabu, hivyo ni wajibu wa jamii inayozunguka katika eneo hilo kuhakikisha wanajenga utamaduni wa kupenda na kuthamini usafi wa mazingira yanayowazunguka ili kulinda afya za watumiaji wa bidhaa na huduma zinazopatikana ndani soko hilo.
Katika hatua nyingine, Mhe. Mtanda amewataka wananchi wa Mkoa huo kujenga utamaduni wa kupanda miti katika maeneo yao kwani kwa kufanya ni kutekeleza amri na maelekezo ya mwenyezi mungu aliyoyatoa katika vitabu takatifu.
Awali akitoa taarifa ya tathimini ya hali ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Afisa Mazingira wa Jiji hilo, Bw. Daudi Joseph amesema katika mwaka 2025/2026 Jiji hilo limefanikiwa kupanda miti 768,476 ambapo miti 176,750 imepandwa na wananchi na wadau wa mazingira.
Ameongeza pia katika kuchagiza suala la utunzaji na uhifadhi wa mazingira, Jiji hilo limeanzisha na kutekeleza kampeni mbalimbali ikiwemo Tunza Mazingira Ng’arisha Nyamagana na kusimamia shughuli za usafi wa mazingira kwa kushirikiana na viongozi wa Jiji hilo.
“Wilaya ya Nyamagana inaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kushirikiana na wadau ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira katika Kata zote 18” amesema Joseph.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Afisa Misitu Mwandamizi Bw. Lucas Sabida ameupongeza Mkoa wa Mwanza kwa juhudi mbalimbali inazoendelea kuzifanya katika kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuhifadhi na kutunza mazingira.
Amesema Ofisi ya Makamu wa Rais imeendelea kupata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa timu ya wataalamu wa Mazingira ya Mkoa huo na kuufanya kuwa ni miongoni mwa Mkoa ya mfano katika uhamasishaji wa jamii kuhusu umuhimu wa kutunza na kuhifadhi mazingira.
Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, 2026 yatafanyika Kitaifa Mkoani Dodoma yakiwa na kauli mbiu isemayo Dira 2050: Tuwajibike Kukijanisha Tanzania.























No comments:
Post a Comment