𝐂𝐂𝐌, 𝐂𝐏𝐂 𝐍𝐀 𝐕𝐘𝐀𝐌𝐀 𝐕𝐘𝐀 𝐔𝐊𝐎𝐌𝐁𝐎𝐙𝐈 𝐀𝐅𝐑𝐈𝐊𝐀 𝐖𝐀𝐈𝐌𝐀𝐑𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐊𝐈𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐎 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Thursday, May 21, 2026

𝐂𝐂𝐌, 𝐂𝐏𝐂 𝐍𝐀 𝐕𝐘𝐀𝐌𝐀 𝐕𝐘𝐀 𝐔𝐊𝐎𝐌𝐁𝐎𝐙𝐈 𝐀𝐅𝐑𝐈𝐊𝐀 𝐖𝐀𝐈𝐌𝐀𝐑𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐊𝐈𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐎

Kibaha, Pwani

CCM leo imekuwa mwenyeji wa mkutano kati ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Vyama Sita Rafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika uliofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS), Kibaha.

Mkutano huo chini ya wenyeji wa Chama Cha Mapinduzi, ulikuwa sehemu ya ziara ya kikazi ya Komredi Liu Haixing, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri wa Idara ya Mambo ya Nje wa CPC kutoka China.

Katika mkutano huo, viongozi wa vyama vya ukombozi kutoka ANC, FRELIMO, MPLA, SWAPO na ZANU-PF walijadiliana na CPC kuhusu kuimarisha mshikamano, kubadilishana uzoefu wa kiuongozi na kusukuma ajenda ya maendeleo ya kisasa kwa ustawi wa wananchi wao.

Viongozi hao pia walishiriki uzinduzi wa Kituo cha Tafiti kuhusu Fikra za Xi Jinping juu ya Ujamaa wenye Maono ya Kichina katika Zama Mpya, hatua inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kielimu na maendeleo kati ya CCM na CPC.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad