NCHI ZA SADC ZAAZIMIA KUIMARISHA ZAIDI USHIRIKIANO WA KIKANDA KUKUZA UCHUMI - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Friday, July 3, 2026

NCHI ZA SADC ZAAZIMIA KUIMARISHA ZAIDI USHIRIKIANO WA KIKANDA KUKUZA UCHUMI

Katibu Mkuu Wizara Fedha Dkt. Natu El- Maamry Mwamba (kulia) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Dharura na Maafa, Wizara ya Afya Tanzania, Dkt. Erasto Sylvanus (kushoto), wakifuatilia kwa makini mijadala katika kikao cha mwisho cha Mkutano wa SADC uliofanyika Harare, Zimbabwe.
-----------------
Na. Eva Ngowi- Zimbabwe

Julai 3, 2026, ilikuwa siku ya mwisho ya Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Fedha na Uwekezaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ambapo nchi wanachama zilihitimisha majadiliano kwa kuwasilisha hoja, mapendekezo na maazimio yaliyolenga kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika sekta za fedha, uwekezaji, afya, maendeleo ya masoko ya mitaji na uthabiti wa uchumi wa Kanda. Maamuzi ya mkutano huo yanatarajiwa kuwasilishwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC unaotarajiwa kufanyika mwezi Agosti, 2026 Durban, Afrika Kusini kwa ajili ya kuridhiwa ili maamuzi hayo yaanze kutekelezwa.

Katika mjadala wa mwisho, wajumbe walisisitiza umuhimu wa kuendelea kuoanisha sera za fedha na uwekezaji, kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa rasilimali fedha na maendeleo, pamoja na kuongeza ushirikiano katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili kanda ili kufanikisha malengo ya Dira ya SADC 2050 na Mpango wa Kimkakati wa Maendeleo wa Kanda –(Reginal Indicative Strategic Development Plan -RISDP 2020–2030).

Mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe kutoka nchi zote 16 wanachama wa SADC ambazo ni Angola, Botswana, Comoro, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Eswatini, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Shelisheli, Afrika Kusini, Tanzania, Zambia na Zimbabwe.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad