𝐎𝐑𝐘𝐗 𝐆𝐀𝐒 𝐙𝐀𝐍𝐙𝐈𝐁𝐀𝐑 𝐘𝐀𝐍𝐎𝐆𝐄𝐒𝐇𝐀 𝐓𝐀𝐌𝐀𝐒𝐇𝐀 𝐋𝐀 𝐊𝐈𝐙𝐈𝐌𝐊𝐀𝐙𝐈,𝐘𝐀𝐊𝐀𝐁𝐈𝐃𝐇𝐈 𝐌𝐈𝐓𝐔𝐍𝐆𝐈 𝐘𝐀 𝐆𝐄𝐒𝐈 𝟐𝟎𝟎 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, August 15, 2026

𝐎𝐑𝐘𝐗 𝐆𝐀𝐒 𝐙𝐀𝐍𝐙𝐈𝐁𝐀𝐑 𝐘𝐀𝐍𝐎𝐆𝐄𝐒𝐇𝐀 𝐓𝐀𝐌𝐀𝐒𝐇𝐀 𝐋𝐀 𝐊𝐈𝐙𝐈𝐌𝐊𝐀𝐙𝐈,𝐘𝐀𝐊𝐀𝐁𝐈𝐃𝐇𝐈 𝐌𝐈𝐓𝐔𝐍𝐆𝐈 𝐘𝐀 𝐆𝐄𝐒𝐈 𝟐𝟎𝟎

Na Mwandishi Wetu ,Zanzibar

ORYX Gas Zanzibar imeeleza hatua mbalimbali inazochukua kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia na katika Tamasha la Kizimkazi kampuni hiyo imetoa mitungi ya gesi 200 huku mkakati kwasasa ni kutoa majenerata yanatotumia gesi ya LPG katika hoteli na viwanda visiwani Zanzibar.

Imesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika matumizi ya LPG na kwamba katika kipindi cha miaka sita matumizi ya nishati safi ilikuwa asilimia sita mwaka 2020 lakini mwaka 2025 ni zaidi ya asilimia 30 ya watumiaji wa nishati safi ya kupikia ya gesi na muamko huo umechangiwa na sekta binafsi,Serikali na wadau wengine.

Akizungumza katika kongamano la nishati safi lililofanyika wakati wa Tamasha la Kizimkazi Zanzibar lililoanza Agosti 12 na kuhitimiswa leo Agosti 14,2026, Meneja Mkuu wa Oryx Gas Zanzibar Shuwekha Khamis amesema kampuni hiyo Oryx wanamchango mkubwa katika matumizi ya nishati safi ya kupikia.

“Hii kazi tumeianza muda mrefu na tumekuwa tukizisaidia taasisi katika mabadiliko na hapa Zanzibar oryx tumeshapiga hatua kuzibadilisha baadhi ya taasisi zikiwemo shule shule 25,Jeshi la Kujenga Uchumi, JKU kuna kambi sita Unguja na Pemba

“Pia kwa kushirikiana na Mwanamke Initiative Foundation tumebadilisha gereza la Kiinua Mguu , vituo vya polisi viwili, vituo vya afya 12 pamoja na baadhi ya ofisi za Serikali na ofisi nyingine.Kwahiyo tunaona kuna hatua kubwa ambayo tumeifanya katika kuzibadilisha taasisi.”

Awali katika tamasha hilo la Kizimkazi Oryx Gas imetoa mitungi ya gesi ya kupikia 250 bure kwa wananchi lengo likiwa kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia hasa kwa kutambua mkakati wa Serikali ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.
------------------------------------------

𝐊𝐀𝐌𝐀𝐑𝐈 𝐍𝐀 𝐊𝐔𝐁𝐄𝐓𝐈 𝐕𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐋𝐈𝐙𝐀 𝐍𝐘𝐔𝐌𝐁𝐀 𝐍𝐀 𝐌𝐀𝐋𝐈 𝐙𝐀𝐍𝐆𝐔 𝐙𝐎𝐓𝐄, 𝐌𝐏𝐀𝐊𝐀 𝐓𝐈𝐁𝐀 𝐘𝐀 𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐈𝐋𝐈𝐏𝐎𝐍𝐈𝐍𝐀𝐒𝐔𝐀 𝐊𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐉𝐀𝐍𝐆𝐀 𝐇𝐈𝐋𝐎.
Kutafuta pesa na kupambania maendeleo ni lengo la kila mtu, lakini pale unapotumbukia kwenye mtego wa michezo ya kubeti na kamari, maisha yote huanza kuporomoka kwa kasi ya ajabu.

Kwa miaka kadhaa, nilikabiliwa na uraibu mzito wa kamari uliyoanza kama mchezo mdogo wa kujiburudisha. Kila nilipoweka pesa na kushinda kiasi kidogo, tamani ya kupata pesa nyingi haraka ilitawala akili yangu, ikanifanya nianze kuweka kiasi kikubwa zaidi cha fedha kila siku.

ENDELEA    KUSOMA

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad