𝐊𝐈𝐇𝐔𝐋𝐋𝐀 𝐀𝐈𝐓𝐀𝐊𝐀 𝐁𝐈𝐀𝐒𝐇𝐀𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐇𝐀𝐖𝐀 𝐌𝐁𝐈𝐍𝐆𝐀 𝐊𝐔𝐙𝐈𝐍𝐆𝐀𝐓𝐈𝐀 𝐕𝐈𝐏𝐈𝐌𝐎 𝐒𝐀𝐇𝐈𝐇𝐈 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Sunday, August 16, 2026

𝐊𝐈𝐇𝐔𝐋𝐋𝐀 𝐀𝐈𝐓𝐀𝐊𝐀 𝐁𝐈𝐀𝐒𝐇𝐀𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐇𝐀𝐖𝐀 𝐌𝐁𝐈𝐍𝐆𝐀 𝐊𝐔𝐙𝐈𝐍𝐆𝐀𝐓𝐈𝐀 𝐕𝐈𝐏𝐈𝐌𝐎 𝐒𝐀𝐇𝐈𝐇𝐈

Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) Bw. Alban Kihulla, Kulia ni Meneja (WMA) Mkoa wa Ruvuma (Nyagabona Mkanjabi) na kushoto ni Meneja wa Kiwanda cha Twende Shamba Tanzania Ltd ( Bw. Ngapomba) 
Vipimo sahihi kwa kutumia mizani iliyohakikiwa na WMA. Kiwanda cha Twende Shamba Tanzania Ltd.

***

Na. WMA – MBINGA, RUVUMA

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA), Alban Kihulla, ametembelea kiwanda cha Twende Shamba Tanzania Ltd kilichopo Mbinga, Mkoa wa Ruvuma, kinachojihusisha na ununuzi wa kahawa kutoka kwa wakulima wadogo pamoja na uchakataji wa zao hilo tarehe 14 Agosti, 2026.

Ziara hiyo imelenga kujionea kwa karibu shughuli za uzalishaji na uchakataji wa kahawa, pamoja na kuhakikisha kuwa vipimo sahihi vinazingatiwa katika kila hatua ya mnyororo wa ukusanyaji wa kahawa.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Kihulla, amesisitiza umuhimu wa matumizi ya vipimo sahihi katika kuhakikisha haki, uwazi na uaminifu katika biashara ya kahawa unazingatiwa, hususan kwa wakulima ambao ni wanufaika wa zao hilo.

“Vipimo sahihi ni msingi wa haki na uwazi katika biashara. Tunapaswa kuhakikisha kuwa kila mdau anapata thamani inayostahili kutokana na bidhaa anayouza au kununua,” alisema Kihulla.

Aidha, ziara hiyo imekuwa sehemu ya juhudi za WMA katika kuimarisha uzingatiaji wa vipimo katika sekta ya kilimo, hatua ambayo ni muhimu katika kuongeza ubora, thamani na ushindani wa zao la kahawa mkoani Ruvuma katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Kahawa ni miongoni mwa mazao muhimu yanayochangia uchumi wa Mkoa wa Ruvuma na Tanzania kwa ujumla. Kwa kuhakikisha usahihi wa vipimo unazingatiwa ipasavyo, WMA inaendelea kuchangia katika kujenga mazingira ya biashara yenye haki, uwazi na manufaa kwa wadau wote, kuanzia mkulima hadi mlaji wa mwisho.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad