𝗠𝗧𝗜: 𝗧𝗨𝗠𝗘𝗔𝗡𝗭𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗦𝗛𝗨𝗟𝗘 𝗭𝗔 𝗔𝗙𝗔𝗣 𝗞𝗨𝗦𝗔𝗜𝗗𝗜𝗔 𝗙𝗔𝗠𝗜𝗟𝗜𝗔 𝗠𝗔𝗦𝗜𝗞𝗜𝗡 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Sunday, August 30, 2026

𝗠𝗧𝗜: 𝗧𝗨𝗠𝗘𝗔𝗡𝗭𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗦𝗛𝗨𝗟𝗘 𝗭𝗔 𝗔𝗙𝗔𝗣 𝗞𝗨𝗦𝗔𝗜𝗗𝗜𝗔 𝗙𝗔𝗠𝗜𝗟𝗜𝗔 𝗠𝗔𝗦𝗜𝗞𝗜𝗡


 Mkurugenzi  wa Shule za Msingi na Sekondari zinazomilikiwa na Kampuni ya AFAP ,  Juma Mti, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kampuni hiyo kuanzisha shule kwa ajili ya kusaidia familia maskini.

........................................

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI wa shule za msingi na Sekondari zinazomilikiwa na Kampuni ya Afap,  Juma Mti, amesema walikusudia ku anzisha shule  hizo kwa lengo la kusaidia yatima na familia maskini ili ziweze kusomesha watoto wao. 

Hayo aliyasema wakati wa mahafari ya tatu ya darasa la saba yaliyofanyika Agosti 29, mwaka huu, Mbondole, Ilala jijini Dar es Salaam.

Wanafunzi wa darasa la saba wanaotarajiwa kufanya mtihani wa Taifa, Septemba 9, mwaka huu.                      

 Mti alisema kuwa lengo za Kampuni ya Afap kuanzisha shule hizo ni kutaka familia ambazo zina  kipato cha chini ziweze kupeleka watoto wao kusoma kwa ada nafuu.

Alisema kuwa lengo la kuweka ada nafuu ni kumwezesha mtoto wa mfanyabiashara anayeuza mbogo mboga au maandazi aweze kumudu kulipa ada hiyo. 

Mti alisema kuwa hakuanzisha shule hizo kwa lengo la kupata faida, bali ni kusaidia familia maskini, ambapo yatima wanasoma bure 

Mkurugenzi huyo alisema kuwa  Kampuni ya Afad  inayomiliki shule tatu ikiwamo ya Sekondari iliyoko  Msimbu, wilayani Kisarawe, mkoani  Pwani  zote zimeanzishwa kwa lengo la kusaidia familia maskini na zinafanya vizuri.

 "Tuna shule tatu, moja ipo hapa Mbondole, Kipawa na nyingine ya Sekondari Msimbu na wanafunzi wetu wanafanya vizuri sana katika mitihani ya Taifa na wengine kuchaguliwa shule bora za serikali," alisema Mti. 

 Kwa upande wa Mkuu wa Shule ya Afap, Iddy Mohammed,  alisema kuwa wanafunzi wao wanafanya vizuri katika mitihani ya Taifa.   

 Mohammed alisema kuwa kutokana na walivyowaandaa wanafunzi wao anaimani wafanya vizuri mtihani wa Taifa ya darasa la saba unaotarajia kuanza Septemba  9, mwaka huu.                           

Pia, alisema kuwa jumla ya wanafunzi 41 wanatarajiwa kufanya mtihani kwa shule hiyo.                                 

Naye, mgeni rasmi ambaye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tawi la Kurutini, Mbondole,  Nasor Ali aliupongeza uongozi wa shule hiyo kwa kuwekeza elimu katika eneo hilo.

 Ali  alifurahishwa na nidhamu ya hali ya juu inayoonyeshwa na  wanafunzi wa shule hiyo                   Amewaomba wazazi kupeleka watoto wao katika shule hiyo ili waweze kupata elimu bora. 

 Akizungumza kwa niaba ya wazazi wa shule hiyo,  Macerina  Nangwachu, aliupongeza uongozi Afap kutokana na kazi nzuri ya kufundisha watoto wao.

 Pia, aliuomba uongozi wa shule hiyo kuanzisha shule ya Sekondari katika eneo hilo la Mbondole ili watoto wao waweze kusoma kwa gharama nafuu.  

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad