𝐒𝐄𝐑𝐈𝐊𝐀𝐋𝐈 𝐈𝐌𝐄𝐓𝐎𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐋𝐈𝐍𝐆𝐈 𝐁𝐈𝐋𝐈𝐎𝐍𝐈 𝟏𝟓𝟔 𝐓𝐀𝐍𝐆𝐀 𝐊𝐔𝐁𝐎𝐑𝐄𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐈𝐔𝐍𝐃𝐎𝐌𝐁𝐈𝐍𝐔 𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐉𝐈𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈𝐀 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Monday, August 17, 2026

𝐒𝐄𝐑𝐈𝐊𝐀𝐋𝐈 𝐈𝐌𝐄𝐓𝐎𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐋𝐈𝐍𝐆𝐈 𝐁𝐈𝐋𝐈𝐎𝐍𝐈 𝟏𝟓𝟔 𝐓𝐀𝐍𝐆𝐀 𝐊𝐔𝐁𝐎𝐑𝐄𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐈𝐔𝐍𝐃𝐎𝐌𝐁𝐈𝐍𝐔 𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐉𝐈𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈𝐀

Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Havian Sanga, akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dk. Batilda Salha Burian, alipotembelea banda la chuo hicho katika Maonesho ya Wiki ya Taifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2026, yanayofanyika katika Viwanja vya Usagara, Jijini Tanga, Agosti 17, 2026.................................

Na Mwandishi Wetu, Tanga

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojiia imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 156 katika Mkoa waTanga kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya kujifunza na kufundishia.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dk. Batilda Salha Burian, alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya Maonesho ya Wiki ya Taifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2026, yanayofanyika katika Viwanja vya Usagara, Jijini Tanga.

Alisema mgeni rasmi wa ufunguzi wa Maonesho hayo ni  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Profesa Adolf Mkenda Agosti 18, 2026.

Alisema maonesho hayo ni jukwaa muhimu linalotoa fursa kwa Tanzania kuweza kujipima kimataifa, huku likionesha mwelekeo wa nchi katika sekta za ufundi, ubunifu na utafiti. 

“ Katika Maonesho haya zaidi ya taasisi 300 zimejitokeza kushiriki huku zikiwasilisha bunifu, tafiti na teknolojia zinazoendana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia duniani,” alisema Burian.

Alizitaja taasisi hizo kuwa ni vyuo vikuu mbalimbali nchini, taasisi za utafiti wa kisayansi na kiufundi, vyuo vya ufundi stadi na vya kati, pamoja na taasisi binafsi zinazojihusisha na masuala ya sayansi, teknolojia na ubunifu.

Balozi Dkt. Burian amewataka wananchi, wataalamu, wanafunzi na wadau wa elimu kujitokeza kwa wingi kushuhudia bunifu mbalimbali na kujifunza teknolojia mpya inazochagiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii hapa nchini.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu na Ufundi stadi (NACTIVET) Mwajuma Lingwanda amesema Baraza hilo limeandaa mashindano ya ujuzi Kitaifa mwaka 2026.

Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Dk. Benson Mugaka akimuelekeja jambo Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dk. Batilda Salha Burian, alipotembelea banda la chuo hicho.
Mbunifu Ibrahim Meshack akitoa maelezo mbele ya Mkuu wa Mkoaa wa Tanga, Dk. Burian.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad