𝗧𝗜𝗖𝗛𝗧𝗘𝗖𝗞 𝗞𝗨𝗔𝗡𝗭𝗔 𝗞𝗨𝗪𝗔𝗧𝗘𝗡𝗚𝗘𝗡𝗘𝗭𝗘𝗔 𝗔𝗝𝗜𝗥𝗔 𝗪𝗔𝗡𝗔𝗙𝗨𝗡𝗭𝗜 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Monday, August 31, 2026

𝗧𝗜𝗖𝗛𝗧𝗘𝗖𝗞 𝗞𝗨𝗔𝗡𝗭𝗔 𝗞𝗨𝗪𝗔𝗧𝗘𝗡𝗚𝗘𝗡𝗘𝗭𝗘𝗔 𝗔𝗝𝗜𝗥𝗔 𝗪𝗔𝗡𝗔𝗙𝗨𝗡𝗭𝗜

 Mkuu wa Shule ya Tichteck, Samwel Semi, akiwa katika mahafali ya darasa la saba, yaliyofanyika Agosti 28, mwaka huu.

Na Mwandishi Wetu. 

           BAADA ya Serikali kuboresha mtala mpya wa elimu nchini. Mkuu wa Shule ya Msingi ya Tichteck iliyoko Mbondole, Ilala, Dar es Salaam, Samwel  Seni, amesema wana mpango wa kujenga bwawa la kufugia samaki kwa lengo la kuwafundisha wanafunzi kwa vitendo ili wakimaliza masomo yao ya darasa la saba waweze kujitegemea katika kujipatia ajira. 

Seni alisema hayo  juzi wakati wa sherehe ya maafali ya tatu ya wanafunzi wa darasa la saba wanaojindaa kufanya mtihani wa Taifa, Septemba, mwaka huu, yaliyofanyika shuleni hapo. 

Alisema kuwa shule yao ina mazingira bora ya kufundishia na wanajenga bwawa la samaki kwa ajili ya kuwafundisha wanafunzi wao kwa vitendo ili wakimaliza shule wasiangaike kutafuta ajira.  

Seni alisema kuwa mipango yao ni kuhakikisha mwanafunzi wa darasa la saba wanaomaliza shuleni hao wanakuwa bora kielimu. 

 Pia alisema kuwa kuanzia mwakani wanafunzi wa shule hiyo wataanza kusoma Tehama  baada ya serikali kuboresha mtala wa elimu nchini. 

Amewataka wazazi kupeleka watoto wao katika shule hiyo ili waweze kupata elimu bora.                                

Mkuu huyo wa shule alisema kuwa wameanza kupokea wanafunzi wapya kwa mwaka 2027 kuanzia umri wa miaka miwili na nusu na ada zao ni nafuu ambazo kila mzazi wanaweza kulipa. 

Kwa upande wake, mgeni rasmi katika maafali hayo, Joseph Opiyo aliwapongeza walimu wa shule hiyo kwa kutoa elimu bora inayozingitia maadili ya Taifa.

Opiyo alisema kuwa amejionea mwenyewe nidhamu ya wanafunzi wa shule hiyo na inatokana na kazi nzuri inayofanywa na walimu wao.

"Nimeshuhudia elimu inayotolewa hapa ni bora sana, wazazi mmejionea hapa jinsi watoto wanavyojielezea mambo yanayosoma darasa tena kwa kichwa tu," alisema Opiyo.

Ametoa wito kwa wazazi  na walezi kutoa ushirikiano kwa walimu ili  kuwajengea mazingira bora watoto wao  kufanya vema darasani. 

Pia amewataka wazazi kuwapeleka watoto katika shule hiyo ili waweze kupata elimu bora.

Wanafunzi wa Tichteck wakielezea jinsi walivyojifunza somo la Sayansi kabla kufanya mtihani wa Taifa wa darasa la saba, Septemba 9, mwaka huu.
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad