Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Aggrey Mwanri, amesema mazungumzo yaliyofanywa na wadau kuhusu hali ya kisiasa nchini yameonyesha mwanga mkubwa juu ya maridhiano na utayari wa wadau katika kupata mwafaka mzuri.
Amesema hayo leo Septemba 7, katika Mkutano wa Kitaifa wa Wadau Kutafakari Hali ya Kisiasa Nchini uliofanyika Serena Hotel, Ujiji Dar es Salaam.
Akieleza kuwa wakati anafika kwenye mkutano alipatwa na wasiwasi akidhani kuwa wadau wangekosoa CCM, vidole vikielekezwa kwa CCM ndiyo sababu lakini mawazo yalikuwa tofauti.
“Wakati nakuja nilikuwa na kahofu kidogo nikafikiria kwamba watarusha mawe CCM bana, chama tawala bana, hii shida yote tunayopata ni CCM bana, tulikuwa na Mzee Wasira nikamwambia kama mood yenyewe ni hii unaweza kuwa na uhakika kuwa tuko tayari,” amesema Mwanri.











No comments:
Post a Comment