𝐌𝐀𝐒𝐀𝐔𝐍𝐈 𝐀𝐓𝐎𝐀 𝐖𝐈𝐓𝐎 𝐊𝐔𝐒𝐈𝐌𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐆𝐈𝐙𝐎 𝐋𝐀 𝐔𝐒𝐀𝐅𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐙𝐈𝐍𝐆𝐈𝐑𝐀 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, September 5, 2026

𝐌𝐀𝐒𝐀𝐔𝐍𝐈 𝐀𝐓𝐎𝐀 𝐖𝐈𝐓𝐎 𝐊𝐔𝐒𝐈𝐌𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐆𝐈𝐙𝐎 𝐋𝐀 𝐔𝐒𝐀𝐅𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐙𝐈𝐍𝐆𝐈𝐑𝐀

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuongoza zoezi la kufanya usafi katika Soko la Buguruni, Jijini Dar es Salaam, Septemba 5, 2026.

PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akizoa taka kwenye toroli la kubebea uchafu wakati akiongoza zoezi la kufanya usafi katika Soko la Buguruni, Jijini Dar es Salaam, Septemba 5, 2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akiongozana na viongozi mbalimbali kufanya usafi katika Soko la Buguruni, Jijini Dar es Salaam, Septemba 5, 2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akisukuma toroli wakati akiongoza zoezi la kufanya usafi katika Soko la Buguruni, Jijini Dar es Salaam, Septemba 5, 2026
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akiweka taka kwenye gari la kubebea uchafu wakati alipoongoza zoezi la kufanya usafi katika Soko la Buguruni, Jijini Dar es Salaam, Septemba 5, 2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akizoa taka kwenye toroli la kubebea uchafu wakati akiongoza zoezi la kufanya usafi katika Soko la Buguruni, Jijini Dar es Salaam, Septemba 5, 2026.
--------------------------

Na; Mwandishi Wetu Dar es Salaam


Serikali inatoa wito kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji  kuhakikisha kuwa wanaweka utaratibu wa kusimamia utekelezaji wa maelekezo ya kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kuwa siku ya usafi  wa Mazingira Kitaifa kwa kuzingatia maslahi ya makundi mbalimbali.  


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni ameyasema hayo mara baada ya kuongoza zoezi la usafi katika Soko la Buguruni Jijini Dar es Salaam, Septemba 5, 2026.


“Tunakumbuka kuwa Serikali kupitia Mheshimiwa Rais akiwa Makamu wa Rais mwaka 2016 alitoa agizo kuwa kila Jumamosi ya mwisho ya mwezi kuwa siku ya usafi  wa Mazingira Kitaifa.


Aidha Ofisi ya Makamu wa Rais ilitoa ‘Enviromental Management (Designation of National Cleanliness Day) Guidelines , 2016,chini ya G.N.No.139. Mwongozo huo unaelekeza utekelezaji wa tamko la Serikali la kuitangaza kila jumamosi ya mwisho wa Mwezi kuwa siku ya usafi wa Mazingira Kitaifa.


“Kwa muktadha huo, Serikali inatoa wito kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji  kuhakikisha kuwa wanaweka utaratibu wa kusimamia utekelezaji wa maelekezo haya kwa kuzingatia maslahi ya makundi mbalimbali.  


“Ni wajibu wa kila mwananchi, mfanyabiashara, mwekezaji, taasisi za Serikali, sekta binafsi, viongozi wa mitaa, wenye viwanda, watoa huduma za taka, taasisi za elimu na jamii kwa ujumla kuwa na utaratibu wa kufanya na kusimamia  Usafi wa Mazingira katika maeneo yao.Hivyo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa tanzania inamtaka kila  Mtanzania kushiriki katika usafi wa mazingira.” Amesema Mhe. Masauni. 


Amesema, taka zinapotupwa hovyo, mifereji inapoziba, maeneo ya biashara yanapokuwa machafu au taka ngumu na hatarishi zinaposhughulikiwa bila utaratibu, madhara yake huonekana katika afya ya wananchi, miundombinu, mito, bahari na uchumi.


Waziri Masauni amesema Mazingira machafu yanaweza kuchangia kuenea kwa magonjwa, kuongeza gharama za usafi na afya, kupunguza mvuto wa miji yetu kwa watalii na wawekezaji, na kuharibu rasilimali ambazo Watanzania wanategemea kwa maisha yao.


 Aidha, usimamizi wa taka hususan katika maeneo ya mjini hairidhishi ambapo wastani wa asilimia 37 tu ya taka ngumu zinazozalishwa hukusanywa na hivyo kiasi kikubwa cha taka huzagaa.


Kwa upande mwingine amesema, taka zinaweza kuwa fursa ya kiuchumi kupitia urejelezaji uchumi rejeshi, taka kutumika kama chanzo cha uzalishaji wa Nishati, Uzalishaji wa mbolea (mboji) na biashara ya kaboni. Mathalani, Tanzania  ina fursa ya uwekezaji wenye thamani ya takribani shilingi bilioni 22 kutoka katika taka plastiki, karatasi chakavu, taka za kielektroniki na betri chakavu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad