Mkurugenzi Msaidizi wa Usalama Mtandao wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Stephen Wangwe akizungumza katika mafunzo ya usalama mtandao kwa Wanafunzi wa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia Zanzibar (KIST) leo Oktoba 25, 2022 .
Mkurugenzi Msaidizi wa Usalama Mtandao wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Stephen Wangwe akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Mafunzo yakitolewa.
.................................................
Na Mwandishi wetu, WHMTH, Zanzibar.
WATANZANIA wameshauriwa kuacha tabia ya kuchapisha picha na video za faragha mtandaoni kwa kuwa ni kinyume na maadili ya kitanzania lakini pia mhusika anaweza kupata madhara ya kisaikolojia kutokana na udhalilishaji anaoweza kuupata mtandaoni.
Mkurugenzi Msaidizi wa Usalama Mtandao wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Stephen Wangwe amezungumza hayo wakati akitoa mafunzo ya usalama mtandao kwa wanafunzi wa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia Zanzibar (KIST) Oktoba 25, 2022 .
Amesema kuwa, matukio ya picha na video za faragha mtandaoni yanazidi kuongezeka na asilimia kubwa zinawekwa bila idhini ya wahusika baada ya kusalitiwa na watu waliowaamini au baada ya kupoteza kifaa cha TEHAMA kilichohifadhi picha hizo.
“Tunapaswa kufikiri kwanza kabla ya kupiga, kurekodi, kutuma na kusambaza matendo ya faragha katika mtandao ili kulinda heshima binafsi na kulinda maadili ya kitanzania”, amezungumza Mhandisi Wangwe
Ameongeza kuwa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015, inazungumza wazi kuwa uchapishaji wa picha au video za faragha mtandaoni (ponography) ni kosa kisheria na adhabu yake ni faini si chini ya milioni 20, au kifungo kisichopungua miaka saba au vyote kwa pamoja.
Mhandisi Wangwe ametoa rai kwa jamii kulinda faragha zao kwa kuhakikisha faragha inabaki kuwa faragha lakini pia kuhakikisha wanalinda vifaa vyao vya TEHAMA kwa kuweka password imara na ikiwezekana zaidi ya moja ili ikitokea kimepotea basi iwe ngumu mtu kufungua au kuona kilichopo ndani.
Naye Mtaalamu wa Usalama Mtandao, Bw. Yusuph Kileo amesema kuwa udhalilishaji wa kimtandao unaongezeka katika jamii na madhara yake ni makubwa sana kwa wahusika ikiwa ni pamoja na msongo wa mawazo au hata vifo hutokea.
“Ni kosa kisheria kudhalilisha watu kwa njia ya mtandao na faini yake si chini ya milioni tano, kifungo cha miaka mitatu au vyote kwa pamoja lakini pia ni muhimu jamii kuhakikisha hatutengenezi mazingira ya kufanyiwa udhalilishaji mtandaoni”, amesisitiza Kileo.
Rashidi Salim Abdallah , mwanafunzi wa TEHAMA wa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia Zanzibar amesema kupitia mada zilizotolewa na wataalamu wa usalama mtandao wamejifunza kujiuliza nini faida ya vitu wanavyoposti mtandaoni na kuepuka vishawishi vya kuwaamini na kuwatumia picha za faragha watu wanaokutana nao na kuanzisha mahusiano mtandaoni.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Tuesday, October 25, 2022
WATANZANIA WAASWA KUACHA KUHAMISHIA FARAGHA MTANDAONI
Tags
# Elimu
Kuhusu - Singidaniblog
Elimu
Tags:
Elimu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
𝗡𝗶 𝗰𝗵𝗼𝗺𝗯𝗼 𝗰𝗵𝗮 𝗵𝗮𝗯𝗮𝗿𝗶 𝗸𝗶𝗻𝗮𝗰𝗵𝗼𝘁𝗼𝗮 𝗵𝗮𝗯𝗮𝗿𝗶 𝗻𝗮 𝗺𝗮𝘁𝘂𝗸𝗶𝗼 𝗺𝗯𝗮𝗹𝗶𝗺𝗯𝗮𝗹𝗶 𝗻𝗰𝗵𝗶𝗻𝗶 𝗧𝗮𝗻𝘇𝗮𝗻𝗶𝗮 𝗻𝗮 𝗸𝗼𝗸𝗼𝘁𝗲 𝗱𝘂𝗻𝗶𝗮𝗻𝗶 ,𝗸𝘄𝗮 𝗸𝘂𝗷𝗮𝗹𝗶 𝘄𝗲𝗹𝗲𝗱𝗶 𝗻𝗮 𝘁𝗮𝗮𝗹𝘂𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗵𝗮𝗯𝗮𝗿𝗶. 𝗞𝗪𝗔 𝗠𝗔𝗧𝗔𝗡𝗚𝗔𝗭𝗢 𝗡𝗔 𝗛𝗨𝗗𝗨𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗛𝗔𝗕𝗔𝗥𝗜, 𝗪𝗔𝗦𝗜𝗟𝗜𝗔𝗡𝗔 𝗡𝗔𝗦𝗜, 𝟬𝟳𝟱𝟰 𝟯𝟲𝟮 𝟵𝟵𝟬. 𝟬𝟲𝟴𝟴 𝟵𝟭𝟰 𝟯𝟰𝟰 𝗘𝗺𝗮𝗶𝗹: 𝘀𝗶𝗻𝗴𝗶𝗱𝗮𝗻𝗶𝟳𝟳@𝗴𝗺𝗮𝗶𝗹.𝗰𝗼𝗺,














No comments:
Post a Comment