MABWENI YACHANGIA WANAFUNZI KUFANYA VIZURI KWENYE MASOMO GEITA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Friday, April 19, 2024

MABWENI YACHANGIA WANAFUNZI KUFANYA VIZURI KWENYE MASOMO GEITA

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mtakuja, ,Constantine Molandi, aliyekuwa kuwa mgeni rasmi, akizungumza kwenye Mahafali ya  pili ya kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Shantamine iliyopo Kata ya Mtakuja mkoani Geita. 

.......................

 Na Joel Maduka, (Singidani Blog)  Geita. 

UWEPO wa Mabweni katika shule za sekondari zimeelezwa kuwa ni moja ya kichocheo cha wanafunzi wa kike kufanya vizuri kwenye masomo yao na kuepukana na vishawishi ambavyo vimekuwa vikiwapelekea kushindwa kutimiza ndoto zao.

Akizungumza kwenye mahafari ya  pili ya kidato cha sita kwenye shule ya Sekondari ya Shantamine iliyopo kata ya Mtakuja,Halmashauri ya Mji wa Geita,Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ambaye pia ni diwani wa Kata hiyo,Constantine Molandi,amesema suala la uwepo wa mabweni umesaidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kufanya vizuri kwenye masomo yao kutokana na kupata muda mrefu wa kujisomea.

“Ukweli uwepo wa mabweni umesaidia kwa kiasi kikubwa sana kuboresha suala la elimu hususani kwa watoto wa kike ukiangalia zamani watoto wengi walishindwa kufikia ndoto zao za kimasomo kutokana na kutembea umbali mrefu kufuata elimu lakini leo hii mfano mzuri ni hapa shantamine watoto wamekuwa wakifurahia na kufanya vizuri kwenye masomo yao kutokana na uwepo wa mabweni na sisi kama halmashauri ni kuona tunaongeza Mabweni mengi zaidi ambayo yatachochea elimu kwa watoto wetu” alisema Molandi.

Nao wazazi na  walimu wameelezea umuhimu wa uwepo wa mabweni shule ambavyo umeendelea kuwa chachu ya ufaulu mzuri kwa wanafunzi.

“Ufaulu shuleni hapa umekuwa ukiongezeka kila mwaka kwanza uwepo wa kidato cha tano na sita  kwetu imekuwa ni fursa kwa wanafunzi wa madarasa ya kuanzia kidato cha kwanza hadi na cha nne  wamekuwa wakitumia kama fursa ya wao kufundishwa masomo ambayo wanaona wanaweza kufundishwa na wanafunzi wenzao,” alisema Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Kakila Swila, 

“Sisi wazazi kwetu imekuwa ni faraja kubwa kuona watoto wetu wanafanya vizuri kutokana na uwepo wa mabweni ya shule ya Sekondari Shantamine,” alisema Yohana Mathias kwa niaba ya wazazi.

Nao wanafunzi wa kidato cha Sita wa shule hiyo ambao wanatarajia kuanza mtihani wao wa kuhitimu kidato cha sita Mei 6, 2024  wameelezea namna walivyojianda kukabiliana na mtihani huo.

“Tunashukuru kwa maandalizi mazuri ambayo walimu wetu wametupatia tunauhakika wa kufanya vizuri pindi tutakapokwenda kufanya mtihani wetu wa kuhitimu kidato cha sita tunamatumaini makubwa ya kwenda kufanya vizuri,” alisema Elina Dison kwa niaba ya wanafunzi wenzake.

 Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Kakila Swila, akizungumza kwenye mahafali hayo.
Viongozi wakiwa meza kuu wakati wa mahafali hayo.
Mahafali yakiendelea.
Mahafali yakiendelea.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Shantamine wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wanafunzi wakiwa kwenye mahafali hayo.
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad