Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Dkt. Hussein Mohamed Omar ametembelea Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu-ADEM kuona utekelezaji wa shughuli zinazotekelezwa na Wakala.Dkt Hussein amefanya ziara hiyo ikiwa ni mara yake ya kwanza kufika ADEM tangu alipoteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu mnamo mwezi Juni, 2025.
NAIBU Katibu Mkuu huyo, amesema lengo la ziara hiyo ni kuifahamu ADEM na kuona shughuli zinazotekelezwa na ADEM ambapo ametumia fursa hiyo kuipongeza Menejimenti ya ADEM kwa utekelezaji wa majukumu ya Wakala kwa ufanisi hususani mafunzo ya uongozi na usimamizi wa elimu yanayolenga kuwajengea umahiri viongozi katika sekta ya elimu kuhusu uongozi na usimamisi wa elimu.
Dkt. Hussein pia amesisitiza Menejimenti ya ADEM kuongeza nguvu katika kufanya tafiti kuhusu mahitaji ya mafunzo ya uongozi na usimamizi wa elimu kwenye shule za Serikali na zile za binafsi yanayolenga usimamizi thabiti wa elimu ya Amali ili kuisaidia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknokojia kutekeleza Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 Toleo la 2023 inayosisitiza utekelezaji wa elimu ya kujitegemea nchini.
“Nimesikia utekelezaji wa shughuli mnazozitekeleza kama Wakala, nawapongeza sana, lakini natoa rai kwa uongozi wa Wakala, jiimarisheni katika kufanya tafiti zinazoendana na muktadha wa usimamizi wa elimu ya Amali inayosisitizwa kwenye Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 Toleo la 2023 ili Wakala uishauri Wizara ya Elimu kuhusu namna bora ya kusimamia eneo la elimu ya Amali, hivyo kuisaidia Wizara kufikia malengo yake katika utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo iliyofanyiwa maboresho.” Amesema Dkt Hussein.
Nae Mtendaji Mkuu wa ADEM Dkt. Maulid J. Maulid akielezea utekelezaji wa shughuli za Wakala kwa Naibu Katibu Mkuu Dkt Hussein amesema ADEM imeendelea kutoa mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi ya Uongozi, Usimamizi na Uthibiti Ubora wa Elimu, kufanya tafiti na kutoa machapisho mbalimbali na kutanabaisha kuwa Wakala pia umejiimarisha katika utoaji wa mafunzo hayo kwa kuanzisha ushirikiano na Taasisi za kimataifa kama vile VVOB-Education for Development na International Institute for Educational Planning – UNESCO.
Aidha, Dkt. Maulid, pia ametumia fursa hiyo kuishukuru Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Mashirika ya Kimataifa kama vile World Bank kupitia miradi mbalimbali ya elimu kwa namna wanavyounga mkono utekelezaji wa shughuli za ADEM.
Katika ziara hiyo, Dkt. Hussein aliambatana na Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw. Sebastian Innosh.
Monday, July 21, 2025
DKT. HUSSEIN: ADEM IBORESHE TAFITI KUHUSU ELIMU YA AMALI
Tags
# Habari
Kuhusu - Singidaniblog
Habari
Tags:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
𝗡𝗶 𝗰𝗵𝗼𝗺𝗯𝗼 𝗰𝗵𝗮 𝗵𝗮𝗯𝗮𝗿𝗶 𝗸𝗶𝗻𝗮𝗰𝗵𝗼𝘁𝗼𝗮 𝗵𝗮𝗯𝗮𝗿𝗶 𝗻𝗮 𝗺𝗮𝘁𝘂𝗸𝗶𝗼 𝗺𝗯𝗮𝗹𝗶𝗺𝗯𝗮𝗹𝗶 𝗻𝗰𝗵𝗶𝗻𝗶 𝗧𝗮𝗻𝘇𝗮𝗻𝗶𝗮 𝗻𝗮 𝗸𝗼𝗸𝗼𝘁𝗲 𝗱𝘂𝗻𝗶𝗮𝗻𝗶 ,𝗸𝘄𝗮 𝗸𝘂𝗷𝗮𝗹𝗶 𝘄𝗲𝗹𝗲𝗱𝗶 𝗻𝗮 𝘁𝗮𝗮𝗹𝘂𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗵𝗮𝗯𝗮𝗿𝗶. 𝗞𝗪𝗔 𝗠𝗔𝗧𝗔𝗡𝗚𝗔𝗭𝗢 𝗡𝗔 𝗛𝗨𝗗𝗨𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗛𝗔𝗕𝗔𝗥𝗜, 𝗪𝗔𝗦𝗜𝗟𝗜𝗔𝗡𝗔 𝗡𝗔𝗦𝗜, 𝟬𝟳𝟱𝟰 𝟯𝟲𝟮 𝟵𝟵𝟬. 𝟬𝟲𝟴𝟴 𝟵𝟭𝟰 𝟯𝟰𝟰 𝗘𝗺𝗮𝗶𝗹: 𝘀𝗶𝗻𝗴𝗶𝗱𝗮𝗻𝗶𝟳𝟳@𝗴𝗺𝗮𝗶𝗹.𝗰𝗼𝗺,










No comments:
Post a Comment