WIZARA ya Nishati kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Umoja wa Ulaya (EU) wamezindua programu ya ushindanishwaji kwa wabunifu katika sekta ya nishati, wakilenga kuchochea mpango wa matumizi bora ya nishati.Imeelezwa kuwa katika ushindanishwaji huo watatafutwa washindi 10 ambao watakuwa na miradi inayochochea matumizi sahihi ya nishati na kuleta suluhu ya changamoto mbalimbali za kijamii katika sekta hiyo, na kwamba kila mshindi atapatia Sh. Milioni 25 hadi 30 kama mtaji wa kuendeleza mradi wake.
Akizungumza leo mkoani Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa program hiyo awamu ya pili, Mwakilishi wa UNDP anaeshughulikia mabadiliko ya tabianchi na nishati, Abas Kitogo, amesema ushindanishwaji huo unahusisha wabunifu wa ndani pekee.
“Watanzania wabunifu wenye teknolojia wanazotaka kuziendeleza wasikose fursa hii, kutafanyika mchakato wa wazi na watakaofanikiwa kupita 20 watapatiwa mafunzo maalum katika kuendeleza bunifu zao, mwaka huu tutaangalia maeneo matatu ikiwemo kuongeza ubunifu katika matumizi bora ya nishati kwenye majengo.
“La pili ni teknolojia ya kuongeza ubora wa vifaa vya nishati vitumike kwa usahihi zaidi, pia teknolojia ya ubunifu kuhusu usambazaji wa taarifa za matumizi sahihi ya nishati katika kubadilisha tabia za watu katika jamii na kuwafanya wawe na uelewa kuhusu matumizi bora,” amesema Kitogo.
Emilian Nyanda, aliyemuwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, amesema mpango wa matumizi bora endelevu ya nishati nchini imesaidia kwa asilimia kubwa kupata nishati ya bei nafuu, utunzaji wa mazingira na kuchochea ukuaji wa uchumi.
Miongoni mwa vijana wanufaika wa mashindano hayo msimu wa kwanza Horrance Pius, ambaye anajihusisha na utengenezaji wa vifaa vya nishati safi na kwamba wamenufaika kutokana na mradi huo ikiwemo kujifunza namna ya kuendesha biashara na kufanikiwa kuingia sokoni.
Naye, Neema Walter, ambaye ni mwanzilishi wa kampuni ya Nishati Next Technology, amesema katika mafunzo waliyopatiwa alifanikiwa kupata ufadhili, pamoja na maarifa yak umuwezesha kuzalisha mashine za kuchakata plastiki, pamoja na majiko.
“Hiyo imenisaidia sana kwani kwa sasa nimepata ukakika wa bidhaa zanga na hata nikiingia sokoni nitakuwa na uwezo wa kushindania na wengine,” amesema.
Tuesday, July 8, 2025
UNDP WAZINDUA MASHINDANO YA UBUNIFU SEKTA YA NISHATI
Tags
# Habari
Kuhusu - Singidaniblog
Habari
Tags:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
𝗡𝗶 𝗰𝗵𝗼𝗺𝗯𝗼 𝗰𝗵𝗮 𝗵𝗮𝗯𝗮𝗿𝗶 𝗸𝗶𝗻𝗮𝗰𝗵𝗼𝘁𝗼𝗮 𝗵𝗮𝗯𝗮𝗿𝗶 𝗻𝗮 𝗺𝗮𝘁𝘂𝗸𝗶𝗼 𝗺𝗯𝗮𝗹𝗶𝗺𝗯𝗮𝗹𝗶 𝗻𝗰𝗵𝗶𝗻𝗶 𝗧𝗮𝗻𝘇𝗮𝗻𝗶𝗮 𝗻𝗮 𝗸𝗼𝗸𝗼𝘁𝗲 𝗱𝘂𝗻𝗶𝗮𝗻𝗶 ,𝗸𝘄𝗮 𝗸𝘂𝗷𝗮𝗹𝗶 𝘄𝗲𝗹𝗲𝗱𝗶 𝗻𝗮 𝘁𝗮𝗮𝗹𝘂𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗵𝗮𝗯𝗮𝗿𝗶. 𝗞𝗪𝗔 𝗠𝗔𝗧𝗔𝗡𝗚𝗔𝗭𝗢 𝗡𝗔 𝗛𝗨𝗗𝗨𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗛𝗔𝗕𝗔𝗥𝗜, 𝗪𝗔𝗦𝗜𝗟𝗜𝗔𝗡𝗔 𝗡𝗔𝗦𝗜, 𝟬𝟳𝟱𝟰 𝟯𝟲𝟮 𝟵𝟵𝟬. 𝟬𝟲𝟴𝟴 𝟵𝟭𝟰 𝟯𝟰𝟰 𝗘𝗺𝗮𝗶𝗹: 𝘀𝗶𝗻𝗴𝗶𝗱𝗮𝗻𝗶𝟳𝟳@𝗴𝗺𝗮𝗶𝗹.𝗰𝗼𝗺,










No comments:
Post a Comment