GULAMALI AAMSHA SHANGWE HARAMBEE YA KUCHANGIA CCM ATOA MILIONI 300 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Tuesday, August 12, 2025

GULAMALI AAMSHA SHANGWE HARAMBEE YA KUCHANGIA CCM ATOA MILIONI 300



Ndugu Haider Gulamali
.........................

Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam

MFANYABIASHARA na Mshindi wa kura za maoni katika kinyang’anyiro cha ubunge Jimbo la Ilongero mkoani Singida Haider Gulamali aliamsha shangwe wakati wa Harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu mwaka huu iliyofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendegu ambaye alikuwa na dharura na kushindwa kuhudhuria kwenye harambee hiyo iliyofanyika     Agosti 12, 2025 Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam  Gulamali alianza kwa kumpongeza Rais Samia na kuimba wimbo maarufu unaoimbwa na wana CCM wa wembe ni uleule ushindi.

Gulamali alihoji wembe huo unatoka wapi na kueleza umetoka kwenye saluni ya CCM na wote waliokuwa wanauimba wamenyolewa na watakuja kuuona tena baada ya miaka mitano ‘akimaanisha waalikwa wote waliohudhuria na kuchangia harambee hiyo.

Akizungumza wakati akichangia harambee hiyo alisema Kampuni ya Africarriers Sh. Milioni 50. Sajjad  Haider Sh. Milioni 25 na mengine Gulamali  Group and Associates Sh. Milioni 125 na mengine kwa pamoja jumla kuu ikiwa ni Sh. Milioni 300.

Katika harambee Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alichangia Sh. Milioni 100.

Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Emmanuel Nchimbi akizungumza na wahariri na waandishi wa habari jijini hapa Agosti 11, 2025  alisema harambee hiyo inalenga kukusanya Shilingi Bilioni 100 kwa ajili ya maandalizi ya kampeni, ikiwemo gharama za magari, mafuta, fulana, mabango, kanga na mambo mengine.

Ndugu Haider Gulamali akiwa katika picha tofauti wakati wa harambee hiyo.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad