..............................................
Mwandishi
Wetu
WAKILI Peter
Madeleka, ameibuka na ushindi katika kura za maoni kuwania kupitishwa na Chama
cha ACT Wazalendo kugombea Jimbo la Kivule.
Iwapo kamati
Kuu ya ACT Wazalendo itampitisha atakuwa mgombea wa Jimbo hilo kupitia Chama
hicho katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba, mwaka huu.
Katika
uchaguzi huo uliofanyika mapema wiki hii, Wakili Madeleka alishinda kwa kupata
kura 38 huku mpinzani wake Colman Marwa akipata kura 12. Hata hivyo, Marwa
atagombea udiwani kata ya Kitunda moja ya kata Sita za Jimbo hilo.
Akitangaza
matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi huo, Risasi Semasaba, alimtangaza pia Nice
Marwa kuwa mgombea Ubunge Viti Maalum Jimbo hilo na mgombea udiwani kata ya
Msongola.
Akizungumza
mara baada ya kutangazwa mshindi, Wakili Madeleka aliwashukuru wapiga kura kwa
kumwamini, akizidi kuwaomba waendelee kumwunga mkono katika safari nzima kwa
kuwa huo ni mwanzo tu.
Kwa upande
wake Marwa baada ya kupewa fursa ya kuzungumza alisema “Ndugu wajumbe nashukuru
sana kwa kura mlizonipa, naomba sasa tuwe pamoja tumwunge mkono Bw. Madeleka.










No comments:
Post a Comment