KIGAMBONI YAITIKA UZINDUZI KAMPENI CCM, ALLY HAPI MGENI RASMI - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, September 6, 2025

KIGAMBONI YAITIKA UZINDUZI KAMPENI CCM, ALLY HAPI MGENI RASMI

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi (kushoto), akiwa meza kuu na viongozi mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa Jimbo la Kigamboni uliofanyika Viwanja vya Mwasongo Kata ya Kisarawe II Jijini Dar es Salaam Septemba 6, 2025. Kulia ni Mgombea Ubunge Jimbo la Kigamboni Haran Sanga na katikati ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigamboni Sikunjema Yahaya.

.......................................

Na Deus Helandogo, Dar es Salaam

SHAMRA shamra, nderemo na vifijo vimeendelea katika Viwanja vya Mwasonga vilivyopo Kata ya Kisarawe II Kigamboni Jijini Dar es Salaam wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kigamboni linazindua kampeni zake za uchaguzi mkuu 2025

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi ndiye mgeni rasmi wa uzinduzi wa kampeni hizo ambazo zimehudhuriwa na maelfu ya wananchi na wana CCM wa Jimbo la Kigamboni na maeneo mengine ya jiji hilo.

Mgombea nafasi ya ubunge wa Jimbo hilo Haran Sanga amekuwa kivutio kikubwa katika uzinduzi huo ambao maandalizi yake yamekamilika kwa viwango vya hali ya juu.

 Uzinduzi huo unahudhuriwa na wagombea nafasi ya udiwani tisa na madiwani wa Viti maalum wanne wa jimbo hilo walioteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kugombea nafasi hizo pamoja na viongozi mbalimbali wa CCM.

 “Uzinduzi huu utanogeshwa na vikundi mbalimbali vya Sanaa na vijana wa hamasa kutoka ndani ya jimbo hilo.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi, akiteta jambo na Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Hadija Saidi.
Mgombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Kigamboni kupitia CCM, Haran Sanga, akiteta jambo na Mwenyekiti wa chama hicho, Wilaya ya Kigamboni, Yahaya Sikunjema wakati wa uzinduzi huo.
Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Wilaya ya Kigamboni, Rehema Kawambwa, akiwa kwenye uzinduzi huo.
Matukio mbalimbali ya hamasa yakiendelea katika viwanja vya Mwasonga.
Hamasa zikiendelea.
Waendesha bodaboda wakiingia kwenye viwanja hivyo.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi, akisalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili kwenye uzinduzi wa kampeni hizo.
Wana CCM wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Kigamboni, Abdallah Pazi akiwajibika.
Nyomi ya Wana CCM wa Wilaya ya Kigamboni wakiwa katika mkutano huo. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad