Maisha ya mtaani yanaweza kukunyanyasa mpaka ukajihisi huna thamani yoyote mbele ya jamii, hasa unapokuwa mwanaume unayekaribia umri wa kuanza familia lakini huna hata mahali pa uhakika pa kulaza kichwa. Naitwa Juma, na kwa miaka mitano nilikuwa nikiishi maisha ya “kupiga chapa” yaani kubahatisha hapa na pale ili nipate mlo wa siku.
Niliingia kwenye ulimwengu wa kubashiri (betting) kwa matumaini makubwa ya kupata mtaji wa kuanzisha maisha, kwani sikuwa na kazi ya kueleweka licha ya kuwa na elimu yangu. Lakini, badala ya kupata ushindi, nilijikuta nimezama kwenye madeni makubwa, na kila mkeka nilioweka ulikuwa unachanika kwa njia za ajabu.
Hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba marafiki na ndugu walianza kunikwepa wakijua nitaomba msaada wa chakula au kodi. Umri wangu wa miaka 34 ulinifanya nijisikie mnyonge, huku kila nikiomba kazi nafasi zinajaa au sipati majibu kabisa










No comments:
Post a Comment