Kulikuwa na tukio la ajabu sana katika mtaa wa Kariakoo jijini Dar es Salaam baada ya kijana mmoja kudaiwa kuingia katika duka la dhahabu kwa nia ya kuiba lakini ghafla kushindwa kutoka nje. Tukio hilo lilivuta umati mkubwa wa watu waliokuwa wakishuhudia hali hiyo ya kushangaza.
Kwa mujibu wa mashuhuda, kijana huyo aliingia dukani kama mteja wa kawaida na kuanza kuangalia mapambo ya dhahabu. Baada ya muda mfupi, alijaribu kuchukua pete moja kwa siri na kuanza kuelekea mlangoni.










No comments:
Post a Comment