WAANDISHI WA KIDIJITALI SINGIDA WAHIMIZWA UBUNIFU KUINUA UCHUMI WAO - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Tuesday, March 24, 2026

WAANDISHI WA KIDIJITALI SINGIDA WAHIMIZWA UBUNIFU KUINUA UCHUMI WAO

Mtendaji Mkuu wa Media Brains, Jesse Kwayu, akitoa mada kwenye mafunzo kwa waandishi wa habari wa kidijitali wa Mkoa wa Singida ya siku mbili yaliyofikia tamati leo Machi 24, 2026 

..............................

Na Dotto Mwaibale, Singida

WANAHABARI wa kidijitali mkoani Singida wametakiwa kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa bidii ili waweze kuinuka kiuchumi kupitia kazi zao. Wito huo umetolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Media Brains, Jesse Kwayu, wakati akitoa mada katika mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari wa kidijitali yaliyohitimishwa Machi 24, 2026 katika Hoteli ya Regency mkoani humo.


Kwayu alisema lengo la msingi la uandishi wa habari si tu kuihabarisha jamii, bali pia kuwawezesha waandishi kupata kipato cha kuendesha maisha yao.


“Lengo la kufanya kazi ya uandishi wa habari ni kuihabarisha jamii pamoja na kupata fedha za kuendeshea maisha,” alisema Kwayu.


Alieleza kuwa kupata kipato kupitia mitandao ya kijamii kunahitaji ubunifu, juhudi na utengenezaji wa maudhui yenye mvuto na yanayokubalika kwa wasomaji. Aliongeza kuwa uandishi wa kidijitali umechukua nafasi kubwa kutokana na kasi ya upatikanaji wa habari, hali inayofanya magazeti ya kuchapishwa kukabiliwa na changamoto ya ushindani kutokana na mitandao ya kijamii kutawala soko.


Akizungumzia matumizi ya Akili Mnemba (AI), Kwayu alisema teknolojia hiyo inarahisisha utendaji wa kazi, lakini waandishi wanapaswa kuhakiki taarifa wanazopata kupitia vyanzo vingine kabla ya kuzichapisha. 


“Akili Mnemba haiwezi kukupa matokeo ya moja kwa moja. Ni jukumu la mwandishi kuhakiki taarifa kabla ya kuisambaza,” alisisitiza.


Kwa upande wake, Afisa Mtendaji wa Media Brains, Absalom Kibanda, alizungumzia umuhimu wa usalama na ulinzi kwa waandishi wa kidijitali wanapotekeleza majukumu yao. Aliwataka kuchukua tahadhari ili kujilinda wao binafsi pamoja na vifaa vyao vya kazi.


Kibanda aliongeza kuwa uandishi wa habari za kidijitali unapaswa kuzingatia taaluma na maadili, akionya kuwa ukiukwaji unaweza kusababisha hatua za kisheria chini ya sheria ya makosa ya kimtandao, ikiwemo faini au kifungo. 


Mafunzo hayo maalum ya kuwajengea uwezo waandishi wa kidijitali mkoani Singida yaliandaliwa na Kampuni ya Media Brains (Brain Incorporated Ltd) ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Konrad Adenauer Stiftung (KAS) Ofisi ya Tanzania

Mkuu wa Uendeshaji wa Media Brains, Absalom Kibanda, akifafanua jambo wakati akitoa mada iliyohusu usalama na ulinzi kwa waandishi wa kidijitali wanapokuwa kazini..

Mratibu wa Mafunzo wa Media Brains, Neville Meena akisisitiza jambo kwenye mafunzo hayo.
Meneja wa Miradi wa Shirika la Konrad Adenauer Tanzania, Damas Nderumaki akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Washiriki wakkifuatilia mada katika mafunzo hayo

 Wanahabari wa kidijitali Mkoa wa Singida wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea
Mratibu wa Mafunzo wa Media Brains, Neville Meena, akimuelekeza jambo mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo
Mwanhabari Edina Alex akiwa kenye mafunzo hayo
Taswira ya mafunzo hayo.
Mshiriki wa mafunzo hayo Michael Ramadhani akiwasilisha moja ya kazi iliyohusu Akili Mnembe wakati wa somo kwa vitendo.
Picha ya pamoja.

Taarifa hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale namba ya simu 0754362990

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad