WANAWAKE SHIVUTA WATOA MSAADA KWA YATIMA, MMILIKI AMLILIA RAIS SAMIA AMPE ARDHI - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Tuesday, March 31, 2026

WANAWAKE SHIVUTA WATOA MSAADA KWA YATIMA, MMILIKI AMLILIA RAIS SAMIA AMPE ARDHI

    Wanawake kutoka Shivuta wakiwa wamekaa na watoto yatima wa kituo cha Ahsante, kilichopo Bombambili, Kivule, Dar es Salaam, baada ya kuwatembelea juzi na kuwapa msaada wa vitu mbalimbali.

...............................

 Na Mwandishi Wetu.      

 WANAWAKE kutoka Shirikisho la Vikundi vya Wajasiliamali Tanzania (SHIVUTA), wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa Kituo cha Yatima kinachojulikana kwa jina la Ahsante Community Tanzania (ACT), kilichopo Bomba Mbili, Kivule, Ilala jijini Dar es Salaam. 

 Wnawake hao kutoka katika shirikisho hilo walitoa msaada wa unga, sembe, sabuni ya kufulia, dawa ya mbu, mafuta ya kupikia, mafuta ya mgando ya kupaka, mchele na viatu. 

Vingine vingine walivyokabidhi ni mabeji ya shule, kalamu, pampasi, biskuti, pipi, nguo za aina mbalimbali, mashuka na madafutari. 

Akizungumza kwa niaba ya watoto hao wakati akipokea msaada huo mwishoni mwa wikiMmiliki wa kituo hicho, Magareth Edward ,  alipaza sauti akimuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kumwezesha kupata ardhi kwa ajili ya upanuzi wa majengo ya kituo huo.                          

"Nawashukuru akinamama wa shivuta kwa kuwatembelea watoto hawa, Mungu awabariki sana, lakini namwomba Rais wetu Samia atusaidie eneo la  ardhi ili tuweze kupanua kituo," alisema Magareth. 

Magareth alisema amelazimika kumwomba Rais Samia msaada huo, kutokana na eneo wanaloishi  watoto wanaolelewa katika kituo hicho ni dogo hawana sehemu ya kucheza. 

Alisema kwa sasa wanaishi katika nyumba ambayo inavyumba vichache na hawawezi kupata nafasi ya kujenga mabweni, viwanja ya michezo na shule kwa ajili yao.

Mmiliki wa kituo hicho, alisema pamoja na ombi hilo kwa Rais Samia, lakini wanachangamoto nyingi, ikiwamo ukosefu wa vitanda, magodoro, shuka na vyoo bora, kwani vilivyopo vinahitaji ukarabati.

Magareth aliongeza kuwa anashindwa kuwatimizia mahitaji yote watoto hao kutokana na hana mtu mwingine wa kumsaidia na hana kipato kikubwa zaidi ya watu wanaoguswa kwa kuwatembelea.                       

Kituo hicho ambacho kina watoto 26, wakiwamo wavula 14 na wasichana 12, baadhi yao wanasoma shule za msingi na sekondari. 

Akikabidhi msaada huo, Afisa Uhusiano wa  Shivuta, Spenciana Ndomba alisema kuwa wanawake shirikisho hilo wameamua kuwatembelea watoto hao kwa sababu wameguswa. 

Wanawake hao wakiwa na watoto hao

Msaada ukitolewa kwa watoto hao.
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad