𝐌𝐇𝐄 𝐁𝐀𝐋𝐎𝐙𝐈 𝐊𝐇𝐀𝐌𝐈𝐒 𝐀𝐓𝐄𝐓𝐀 𝐍𝐀 𝐔𝐉𝐔𝐌𝐁𝐄 𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐓𝐄𝐑𝐀𝐈𝐃 𝐔𝐊 𝐍𝐂𝐇𝐈𝐍𝐈 𝐊𝐎𝐍𝐆𝐎 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Thursday, May 28, 2026

𝐌𝐇𝐄 𝐁𝐀𝐋𝐎𝐙𝐈 𝐊𝐇𝐀𝐌𝐈𝐒 𝐀𝐓𝐄𝐓𝐀 𝐍𝐀 𝐔𝐉𝐔𝐌𝐁𝐄 𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐓𝐄𝐑𝐀𝐈𝐃 𝐔𝐊 𝐍𝐂𝐇𝐈𝐍𝐈 𝐊𝐎𝐍𝐆𝐎

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), (kulia) akiwa katika picha na Mkurugenzi Mtendaji wa WaterAid UK-Kanda ya Kusini mwa Afrika, Bw. Robert Kampala, baada ya kufanya kikao cha kujadili ushirikiano kati ya Tanzania na Taasisi hiyo katika kufadhili Sekta ya maji, pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa 61 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Mkutano Mkuu wa 52 wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki hiyo (ADF), unaoendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kintele, Jijini Brazzaville, katika Jamhuri ya Kongo.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (Katikati), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa pili kulia), Kaimu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, ambaye pia ni Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade (kushoto),  Mkurugenzi Mtendaji wa WaterAid UK-Kanda ya Kusini mwa Afrika, Bw. Robert Kampala (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Pan Africa Advocacy wa WaterAid UK, Dkt. Tanko Yussif Azzika (Kulia), wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao chao kilichojadili ushirikiano kati ya Tanzania na Taasisi hiyo katika kufadhili Sekta ya maji, pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa 61 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Mkutano Mkuu wa 52 wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki hiyo (ADF), unaoendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kintele, Jijini Brazzaville, katika Jamhuri ya Kongo.
------------------------------

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao na Ujumbe wa Taasisi ya WaterAid UK, ukiongozwa na Mkurugenzi wake Mtendaji wa Kanda ya Kusini mwa Afrika, Bw. Robert Kampala, Mkutano uliofanyika pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa 61 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Mkutano Mkuu wa 52 wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki hiyo (ADF), unaoendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kintele, Jijini Brazzaville, katika Jamhuri ya Kongo.


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na WaterAid UK zimeahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimkakati ili kuendeleza huduma endelevu za Maji, Usafi wa Mazingira, na Usafi wa Binafsi (WASH).


Ushirikiano huo unalenga kuimarisha mifumo ya kitaasisi, kutekeleza miradi, na kupanua uwekezaji unaohimili mabadiliko ya tabianchi ili kuongeza kasi ya maendeleo ya sekta hiyo.


Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, ambaye pia ni Gavana Mbadala (Alternate Governor) wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kaimu Naibu Katibu Mkuu ambaye pia ni Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, na Bw Robert Mtengule, ambapo kwa upande wa WaterAid UK, alikuwepo Mkurugenzi wa Pan Africa Advocacy, Dkt. Tanko Yussif Azzika na maafisa wengine wa Wizara ya Fedha.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad