𝐓𝐈𝐀 𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈𝐃𝐀 𝐘𝐀𝐓𝐎𝐀 𝐖𝐀𝐇𝐈𝐓𝐈𝐌𝐔 𝐖𝐀 𝐊𝐖𝐀𝐍𝐙𝐀 𝐒𝐇𝐀𝐇𝐀𝐃𝐀 𝐘𝐀 𝐔𝐙𝐀𝐌𝐈𝐋𝐈 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, June 6, 2026

𝐓𝐈𝐀 𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈𝐃𝐀 𝐘𝐀𝐓𝐎𝐀 𝐖𝐀𝐇𝐈𝐓𝐈𝐌𝐔 𝐖𝐀 𝐊𝐖𝐀𝐍𝐙𝐀 𝐒𝐇𝐀𝐇𝐀𝐃𝐀 𝐘𝐀 𝐔𝐙𝐀𝐌𝐈𝐋𝐈

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego ambaye alikuwa mgeni rasmi akifungua program ya mafunzo ya Uzamili ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida ambayo kwa mara ya kwanza imetoa Wahitimu wa Shahada ya Uzamili katika mahafali ya kihistoria yaliyofanyika Juni 5, 2026.

..............................

TAASISI ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida kwa mara ya kwanza imetoa Wahitimu wa Shahada ya Uzamili katika mahafali ya kihistoria.

Katika Mahafali hayo ya 24  wahitimu 548 kutoka Kampasi za Dar es Salaam, Zanzibar, Mtwara, Kigoma na Singida wametunukiwa Shahada za Uzamili.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego ambaye alikuwa mgeni rasmi akifungua program ya mafunzo ya uzamili Juni 5, 2026 alisema mahafali hayo ni hatua muhimu kwa mkoa wa Singida katika kuendelea kuzalisha wataalamu bobezi wanaohitajika katika sekta mbalimbali za umma na sekta binafsi.

“Wakati tunaianza hii safari na mimi nilikuwemo hivyo ni sehemu ya mafanio haya ambayo yametoa fursa kwa wana Singida hasa watumishi wa umma kuweza kujiendeleza na leo tunaona ushuhuda wa watumishi waliotoka maeneo mbalimbali katika mkoa wetu wa Singida,” alisema Dendego.

Dendego aliwaambia wahitimu hao kuwa mafanikio hayo wanayosherehekea ni ya kitaaluma ambayo yametokana na bidii, juhudi, nidhamu, uvumilivu na kujituma kwao katika kutafuta elimu.

Alisema kwa kufanya hivyo wametimiza maamurisho ya Mwenyezi Mungu ambaye amesema kwenye vitabu vyote vya dini kuwa wsimuache elimu akaenda zake na waaende popote pale hata uchina hivyo wametekeleza maagizo hayo.

Aidha, alisema wametekeleza mapendekezo na malengo ya Serikali nay a familia zao hivyo anawapongeza kwa hatua hiyo ambayo wameifikia na kuwa siyo mwisho wanahitaji kusonga mbele hadi wafike juu kabisa.

Dendego aliwaambia wahitimu hao kuwa kila kizazi hupewa jukumu lake na jukumu la kizazi chao ni kuhakikisha Tanzania inanufaika na mapinduzi ya teknolojia, maarifa na ubunifu unaoendelea kote duniani kwa kuleta tija, ushindani na fursa ya maendeleo ya haraka kwa ajili ya kuendeleza maendeleo ya wananchi, jamii na Taifa kwa ujumla.

“Naamini elimu mliyopata imewafanya kujitambua nan i tegemeo la taifa lisiloona mdudu rushwa nendeni mkakae mbali na mambo haya, mkatusaidie kuyapiga vita ili tuwe na jamii salama wakati wote, inaumiza sana kuona muhitimu wa levo yenu anaenda kuipeleka kwenye uraibu, kupelekwa kwenye vyombo vya dola kwa sababu ya rushwa na amini haya yote mmesisitizwa na taifa linawategemea,” alisema Dendego.  

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Profesa William Pallangyo akitoa taarifa kwenye mahafali hayo alisema katika mahafali hayo ya 24 Wahitimu 548 wametunukiwa shahadi hiyo kutoka Kampasi za Dar es Salaam, Zanzibar, Mtwara, Kigoma na Singida.

Alisema kati ya wahitimu hao, wanawake ni 264 sawa na asilimia 48, na wanaume ni 284 sawa na asilimia 52.

Alisema Jumla ya wahitimu 177 wa kampasi za Dar es Salaam, Zanzibar, na Singida, wametunukiwa Shahada ya Uzamili. Kati ya hao, wanawake ni 56 sawa na asilimia 32 na wanaume ni 121 sawa na asilimia 68.

Alisema Wahitimu wengine 371 kutoka kampasi za Dar es Salaam, Mtwara na Kigoma, wametunukiwa Cheti cha Awali, Astashahada na Stashahada.

“Nawapongeza wahitimu wote kwa juhudi, nidhamu na uvumilivu walioonesha hadi kufikia hatua hii muhimu katika maisha ya kitaaluma,” alisema Profesa Pallangyo.

Akizungumzia mafanikio ya Kampasi ya Singida alisema Taasisi imeendelea kupiga hatua kubwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya msingi sambamba na uboreshaji wa miundombinu ya kufundishia na kujifunzia. 

Profesa Pallangyo alisema mafanikio hayo yanatekelezwa kupitia ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samiaa Suluhu Hassan kupitia Mradi wa Mageuzi ya Kiuchumi kwa Vyuo vya Elimu ya Juu (HEET) kwa usimamizi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. 

Miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana ni u jenzi wa Jengo la Taaluma katika Kampasi ya Singida ambalo limegharimu Shilingi bilioni 13.5 ambao ujenzi wake umefikia asilimia 60.

Aidha, aliongeza kuwa Kampasi ya Mwanza kuna ujenzi wa hosteli mbili za wanafunzi ambapo ujenzi wake umegharimu Shilingi bilioni 7.2 na umefikia asilimia 95 ya utekelezaji.

Alisema Taasisi ya Uhasibu Tanzania ina miradi mingine ya ujenzi wa Majengo ya taaluma na utawala katika Kampasi ya Kigoma ambayo inagharimu Shilingi bilioni 11.08 na yamekamilika kwa asilimia 98.

Akizungumzia ujenzi wa majengo ya taaluma, utawala na mabweni katika Kampasi ya Zanzibar ambayo yamegharimu Shilingi bilioni 15.9 alisema ujenzi wake umefikia asilimia 30 ya utekelezaji. 

Kukamilika kwa miundombinu hiyo, kutaiwezesha Taasisi hiyo kuongeza udahili sambamba na ubora wa huduma za mafunzo.

Alisema kwa mwaka 2025/2026 Taasisi hiyo imefanya zaidi ya tafiti 13 na kuzalisha machapisho 60 ya kitaaluma katika maeneo mbalimbali.

Profesa Pallangyo aliongeza kuwa Watumishi 24 wanaendelea na masomo ya Shahada ya Uzamivu (PhD) katika vyuo mbalimbali nchini na nje ya nchi.

Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi Renetus Msangira akimwakilisha Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara alisema kuhitimishwa kwa kundi la kwanza la Shahada ya Uzamili katika Kampasi ya Singida ni hatua muhimu katika kuongeza fursa za elimu ya juu nchini.

Alisema Bodi ya Ushauri ya Wizara, itaendelea kusimamia na kuunga mkono juhudi za kuhakikisha Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) inabaki kuwa taasisi ya mfano katika utoaji wa elimu, utafiti na ushauri wa kitaalam.

Msangira alitumia nafasi hiyo kutoa shukukrani kwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kuendelea kuimarisha sekta ya elimu ya juu nchini kupitia uwekezaji katika miundombinu, rasilimali watu, Mifumo ya TEHAMA na mazingira bora ya kujifunzia katika Taasisi hiyo ya Uhasibu Tanzania.

Akitoa nasaha kwa Wahitimu Msangira alisema elimu waliyopata ni zaidi ya cheti au shahada.

“Elimu mliyopata ni dhamana ya kutumia maarifa, ujuzi na weledi wenu, kuleta mabadiliko chanya katika jamii,” alisema Msangira.

 Imeandaliwa na Mtandao wa singidaniblog.co.tz

Simu namba: 0754 362990 / 0688 914 344

👇TAZAMA  VIDEO HAPA  CHINI 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Profesa William Pallangyo akitoa taarifa kwenye mahafali hayo.Mjumbe wa Bodi Renetus Msangira kwa niaba ya  Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara, akizungumza.Mshereheshaji (MC) wa mahafali hayo, Imani Matonya akiwajibika.Mkurugenzi wa TIA Kampasi ya Singida Dkt. James Mrema, akizungumza.Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayoMahafali yakiendeleaNdugu ,Jamaa, Marafiki na Wazazi wa Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego ambaye alikuwa mgeni rasmi akiwa na viongozi wengine meza kuu. Kulia ni Prof. Momole Kasambala, Makamu Mkuu wa Chuo - Taaluma, Utafiti na Ushauri na Mkurugenzi wa TIA Kampasi ya Singida, Dkt. James Mrema.Mahafali yakiendeleaWahadhiri wakiwa kwenye mahafali hayoMgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego akiagana na viongozi mbalimbali.Wafanyakazi wa TIA Kampasi ya Singida wakiwa katika ubora wao kwenye mahafali hayo.Picha ya Pamoja

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad