𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀𝐍𝐈 𝐇𝐀𝐍𝐃𝐄𝐍𝐈 𝐖𝐀𝐌𝐄𝐓𝐀𝐊𝐈𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐋𝐈𝐏𝐀 𝐊𝐎𝐃𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐇𝐈𝐀𝐑𝐈 𝐁𝐈𝐋𝐀 𝐒𝐇𝐔𝐑𝐔𝐓𝐈 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Monday, June 8, 2026

𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀𝐍𝐈 𝐇𝐀𝐍𝐃𝐄𝐍𝐈 𝐖𝐀𝐌𝐄𝐓𝐀𝐊𝐈𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐋𝐈𝐏𝐀 𝐊𝐎𝐃𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐇𝐈𝐀𝐑𝐈 𝐁𝐈𝐋𝐀 𝐒𝐇𝐔𝐑𝐔𝐓𝐈

Na Hamida Kamchalla, HANDENI.

WANANCH wilayani Handeni wametakiwa kulipa kodi kwa hiari bila shuruti ili kuchangia ukuaji wa pato la Wilaya hiyo na Taifa Kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Huduma za Kodi katika kata ya Mkata, wilayani, Mkuu wa Wilaya ya Handeni Salum Nyamwese amesema ulipaji wa kodi ni wajibu wa kila mwananchi anayestahili na kwamba mapato hayo ndiyo msingi wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
TAZAMA VIDEO  HAPA
Kwa upande wake, Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga, Castro John, amesema kuanzishwa kwa kituo hicho kunalenga kuboresha utoaji wa huduma za kodi kwa wananchi na wafanyabiashara wa eneo la Mkata na maeneo jirani, baada ya wananchi kulazimika kusafiri takribani kilomita 90 kufuata huduma hiyo.

Nae Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Tanga Ismail Masoud amewataka wafanyabiashara kuendelea kujenga mahusiano mazuri na TRA kwa kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi nakupongeza hatua ya TRA kuwafikia wafanyabiashara wadogo katika maeneo yao huku Mwenyekiti wa Chama Cha wafanyabiashara Wajasiriamali Mkoa wa Tanga Aziza Mfinanga akitoa rai kwa Wajasiriamali kufika katika kituo hicho ili kupata elimu juu ya masuala ya Kodi.

Wilaya ya Handeni imewataka wananchi wanaojihusisha na shughuli za kiuchumi kupitia vikundi mbalimbali kuhakikisha wanajisajili kisheria katika mifumo ya walipa kodi ili watambulike rasmi na kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad