WAKAZI BUYUNI WAMPONGEZA MGANGA MFAWIDHI - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Friday, June 26, 2026

WAKAZI BUYUNI WAMPONGEZA MGANGA MFAWIDHI

 Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Buyuni, Faraji Chwango

.....................................

Na Mwandishi Wetu.      

 WAKAZI wa Kata ya Buyuni, Ilala jijini Dar es Salaam, wamempongeza Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Buyuni, Faraji Chwango, kutokana na kusimamia vyema huduma ya afya. 

Kwa sasa Zahanati ya Buyuni imepandishwa hadhi na kuitwa kituo cha afya.  

Wakizungumza juzi kwenye mkutano wa wananchi katika shina namba tatu la Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Khalfan Said, alisema kuwa kutokana na huduma bora inayotolewa hospitalini hapo kuna haja ya kumpongeza mfawidhi na wahudumu wake wengine.

Said alisema kwa sasa huduma ya afya imeboreka tofauti na zamani kabla ya ujio wa Chwango.               

 "Tunampongeza mfawidhi kwa kazi nzuri , sisi wanabuyuni tunafarajika na huduma na zahanati yetu," alisema Said.  

Alisema kuwa kutokana na huduma bora katika zahanati hiyo, inawafanya wasiende kupata matibabu katika hospitali za mbali. 

Kwa upande wake, Mariam Shamte, alisema kuwa kuwapo kwa huduma bora katika zahanati hiyo, kuwapunguzia gharama  ya kufuata matibabu umbali mrefu. 

"Kwa kweli tunampongeza mfawidhi wetu kwa huduma nzuri katika zahanati yetu, leo hii imepandishwa hadhi ya kuitwa kituo cha afya, tunashukuru sana," alipongeza.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Buyuni, Sylivanus Mwenda, alisema kuwa zahanati yao imepewa tuzo kutokana utendaji mzuri.

Mwenda alisema kuwa Zahanati ya Buyuni ni kati zahanati bora iliyopewa tuzo mwaka jana.                                

Mwenyekiti huyo, alisema kuwa kwa sasa huduma ya afya itapatikana kwa saa 24, baada ya serikali kuipandisha hadhi zahanati yao kwa kuitwa kituo cha afya Buyuni.

"Kuanzia sasa huduma ya afya itapatikana saa 24, tayari duka la dawa lipo pale, jengo la upasuaji na hodi ya mama na mtoto limejengwa," alisema Mwenda. 

Aliwataka wakazi wa Buyuni kwenda kupata huduma ya afya katika kituo hicho.    

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad