WAKAZI HOMBOZA KICHANGANI WAMUOMBA RAIS KUSIKILIZA KILIO CHAO - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, June 13, 2026

WAKAZI HOMBOZA KICHANGANI WAMUOMBA RAIS KUSIKILIZA KILIO CHAO

          Wakazi wa Homboza Kichangani wakizungumzia mgogoro huo.

....................................................    

Na Mwandishi Wetu.         

ZAIDI ya kaya 200 zinazoishi katika Kitongoji cha Homboza Kitongoji, Kata Msimbu, zimemwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kuingilia kati mgogoro wa ardhi baina yao na Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani. 

Mgogoro huo umekuja baada ya Halmashauri kudai, eneo hilo ni mali ya Serikali na wakazi wa Kitongoji hicho walivamia na kujenga nyumba. 

Kutokana na kuwepo kwa mgogoro huo ulioibuka kuanzia mwaka jana, wakazi wa Homboza Kichangani wamemwomba Rais Samia kufika katika eneo ili aweze kusikiliza kilio chao. 

Wakizungumza katika eneo hilo la Homboza Kichangani, mmoja wa wakazi hao, Ramadhani Hamb alidai chanzo cha mgogoro huo ni viongozi wa Halmashauri na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti. 

Ramadhani alidai kuwa ameishia katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka 15, lakini Halmashauri wamepima viwanja wakitakiwa walipie kwa square meta sh. 2500 kwa muda wa miezi mitatu.                                 

Alidai wakishindwa  kulipa kiasi hicho cha fedha, wameambiwa waondoke wenyewe na washindwa kufanya hivyo nyumba zao zitabomolewa na serikali. 

Kwa upande wake, Jumanne Fuki, alidai kabla ya eneo hilo, kupimwa viwanja walifika Magoti na kuwaeleza wangerasimishiwa maeneo yao, baadaye aliwageuka.

Kufi alidai baada ya kurasimishiwa ardhi yao, mkuu wa wilaya Magoti alikuja na mradi wa kupima viwanja na sasa wanauziwa square meta kwa sh. 2500, kinyume na makubaliano yao, kwani kiasi hicho ni kikubwa kwa maishi ya wakazi wa Homboza Kichangani. 

Kutokana na hilo, wamemwomba Rais Samia kufika katika eneo hilo ili aweze kusikilia kero zao.           Naye, Christian Nkwela, alidai kuwa ameishi Homboza Kichangani Kwa miaka 18, lakini kwa kipindi hicho hawakuwahi kuguswa na mtu yeyote.

Nkwela alidai kwa kipindi hicho wanapata huduma zote kutokana serikalini kama wananchi wengine wa Tanzania, lakini kuanzia mwaka jana walianza kusumbuliwa na Magoti.

Alidai maeneo waliyojenga nyumba walipewa na serikali ya Kitongoji cha Homboza na muda wote hapakuwa na mgogoro.   Pia alidai eneo hilo, lingekuwa la mwekezaji serikali ya Kitongoji isingekubali wananchi wanunue ardhi na kujenga shule ya msingi  Kichangani. 

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sika Sika,  alikiri kuwapo kwa mgogoro huo, lakini akishauri kuwepo mjadala mpana.

Sika, alisema serikali ya Kisarawe ikiendelea kufuata sheria itawaumiza wananchi. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kisarawe, Nyahori Mahumbwe, alipouliza kuhusu sakata hilo,  alikataa kuzungumzia chochote kwa kuwa linaratibiwa na mkuu wa wilaya hiyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya Kisarawe, Magoti alisema eneo hilo, lenye ukubwa wa square meta 3000 lilirudishwa serikalini mwaka 2018 na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati John Magufuli, baada ya mwekezaji Palaray kushindwa masharti ya kuendeleza ardhi hiyo.  

Magoti alisema alipofika Kisarawe alikuta eneo hilo, limevamiwa na madalali wa kuuza viwanja na tayari nyumba 721zilikuwa zimejengwa. 

Alisema baada ya serikali kuliona hilo ikaona si vizuri kuwafukuza wakazi hao na ikaja na mpango wa kuwarasimishia ardhi yao kwa kuwataka kulipia square meta kwa sh 2500 kuliko kuwapa bure.                 

Mkuu huyo alisema kuwa baadhi ya watu wameanza kulipia na wanaomalalamika ni wale ambao hawana uwezo wa kulipia na wakishindwa watanyang'anywa viwanja vyao.   

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad