𝐃𝐂 𝐈𝐑𝐀𝐌𝐁𝐀 𝐀𝐊𝐀𝐁𝐈𝐃𝐇𝐈 𝐉𝐄𝐍𝐆𝐎 𝐋𝐀 𝐎𝐅𝐈𝐒𝐈 𝐘𝐀 𝐓𝐀𝐍𝐄𝐒𝐂𝐎 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Monday, July 6, 2026

𝐃𝐂 𝐈𝐑𝐀𝐌𝐁𝐀 𝐀𝐊𝐀𝐁𝐈𝐃𝐇𝐈 𝐉𝐄𝐍𝐆𝐎 𝐋𝐀 𝐎𝐅𝐈𝐒𝐈 𝐘𝐀 𝐓𝐀𝐍𝐄𝐒𝐂𝐎

Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda (katikati), akikata utepe kuashiria kukabidhi rasmi jengo la Ofisi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wilaya hiyo mkoani Singida Julai 4, 2026 baada ya ujenzi wake kukamilika.

...............................

MKUU wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda amekabidhi rasmi jengo la Ofisi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wilaya hiyo mkoani Singida baada ya ujenzi wake kukamilika.


Ujenzi wa jengo hilo lililojengwa na shirika hilo umegharimu Shilingi Milioni 285 na ujenzi wa mradi huo ulianza Novemba 28, 2025.


Akizungumza Julai 4, 2026 kabla ya kukabidhi jengo hilo  Mwenda aliipongeza Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa maboresho makubwa ya miundombinu ya umeme hasa ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere.


Alisema siyo nchi nyingi katika Bara la Afrika na hata nje ya Afrika ambazo zimefika ilipofika Tanzania kwenye suala zima la uzalishaji na usambazaji umeme ni mafanikio makubwa.


Mwenda alisema miaka 30, 20 na 15 iliyopita hali ya hupatikanaji wa umeme ilikuwa ni kizungumkuti na kukaa wiki bila ya kupata umeme ilikuwa jambo la kawaida.


“Kwa wiki ilikuwa tunapata umeme kwa siku tatu tu tena usiku lakini leo hii katika nchi yetu haiwezi ikapita siku nzima bila ya umeme kukosekana kuwaka sasa ni miaka minne na hiyo yote ni kwa sababu ya maboresho yaliyofanyika,” alisema Mwenda.

 

Alisema Tanesco ilikuwa na madeni makubwa ambayo ilikuwa mzigo kwa Serikali na kwa shirika lenyewe leo hii kwa sehemu kubwa madeni hayo yamepunguzwa kwa kiwango kikubwa.


Mwenda alisema hali hiyo ilitokakana na kukodi mitambo na kukunua umeme uliozalishwa na matumizi ya mitambo iliyokuwa ikitumia dizeli kwa gharama kubwa.


“Leo tunazalisha umeme wenyewe baada ya kujenga Bwawa la Mwalimu Nyerere kwa fedha zetu wenyewe kutokana na maamuzi magumu aliyoyafanya Rais wa Tano wa nchi yetu Hayati Dk. John Pombe Magufuli ili ni jambo la kujipongeza,” alisema Mwenda.

 

Aidha, Mwenda alisema Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya miaka mitano iliyopita imeeleza kuwa tayari Tanzania imesambaza umeme kwa asilimia 51 na imebaki asilimia 49 kwenye vitongoji na kuwa kwenye miji, mitaa na vijiji vyote vina umeme na vimebakia vitongoji 31, 320 kwa nchi nzima.


Alisema kwa Wilaya Iramba walikuwa na vitongoji 243 ambavyo vilikuwa na umeme kati ya vitongoji 393, vitongoji zaidi ya 150 havikuwa na umeme mpaka mwaka jana lakini kutokana na mpango mzuri wa Serikali tayari amepatikana mkandarasi kwa ajili ya kuweka umeme kwenye vitongji 50.


Mwenda aliongeza kuwa pia kuna mkandarasi mwingine anaendelea kuunganisha umeme kwenye vitongji 18 ambapo ameeleza kuwa ndani ya miaka mitatu wilaya hiyo vitongoji vyote vitakuwa na umeme.


Kwa upande wake Meneja wa shirika hilo Mkoa wa Singida, Mhandisi Mwamvita Ally alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha fedha za ujenzi wa jengo hilo la ofisi ya wilaya ambalo linakwenda kuboresha mazingira ya Wafanyakazi waweze kuifanya kwa ubora na Wananchi waweze kuhudumiwa kwenye ofisi yenye hadhi. 


Aidha, Mwamvita aliipongeza timu iyofanikisha ujenzi wa jengo hilo ambayo aliiongoza na kufanikisha kumaliza ujenzi wake ndani ya miezi sita.


Akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi huo Meneja wa shirika hilo Wilaya ya Iramba, Idefonce Arthur alisema ujenzi wa mradi huo ulianza kwa kazi ya kung’oa visiki na kusafisha eneo la ujenzi huku mpango kaziukiwa likamilike Juni 30, 2026.


Alisema jengo hilo lina ofisi ya Wafanyakazi, Huduma kwa Wateja pamoja na Ukumbi wa  mikutano na Mitambo ya TEHAMA na kuwa mradi huo umefikia asilimia 98 ya utekelezaji.


Akizungumzia manufaa ya mraadi huo alisema utaboresha mazingira ya kazi kwa Watumishi na kuongeza ufanisi wa huduma na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa Wananchi wa Wilaya ya Iramba. 


Alisema pia ofisi hiyo itatumika kama kichocheo cha kuwasaidia na kuhamasisha wananchi kutumia njia mbadala kama hatua ya kukabiliana matumizi ya kuni na mkaa kwa maendeleo endelevu.


Arthur alisema ofisi hiyo itasaidia kupunguza gharama kwa shirika kwa kuokoa kodi ya kupanga jengo na usumbufu kwa wateja pale eneo la ofisi linapobadilika mara kwa mara.


Aliongeza kuwa ujenzi wa mradi huo ulisaaidia kutoa ajira kwa wananchi wa maeneo ya Kiomboi na kuwa mpango wa baadaye ni kuhakikisha jengo hilo linakuwa kitovu cha kutoa huduma bora, utawala bora na ufanisi wa Taasisi kwa muda wote kuboresha kwa kuweka fenicha na ujenzi wa uzio.


Meneja huyo alitumia nafasi hiyo kumshukuru Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Dk. Mwigulu Mchemba kwa utekelezaji wa ilani ya CCM kwa vitendo.Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda, akizungumza wakati wa kukabidhi ofisi hiyo. Kulia ni Meneja wa TANESCO Mkoa wa Singida Mhandisi Mwamvita Ally.Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda, akikata keki maalumu wakati akikabidhi jengo hilo.Meneja wa TANESCO Mkoa wa Singida Mhandisi Mwamvita Ally akizungumza.Meneja wa shirika hilo Wilaya ya Iramba, Idefonce Arthur, akitoa taarifa yaa ujenzi wa jengo hilo.Wafanyakazi wa shirika hilo wakiwa kwenye hafla hiyo.Hafla ikiendelea.Hafla ikiendelea.Muonekano wa keki maalumu ya kukabidhi jengo hilo.Muonekano wa jengo la ofisi hiyo. Picha ya pamoja

......................................

Taarifa hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale simu namba 0754362990

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad