𝐌𝐂𝐇𝐔𝐍𝐆𝐀𝐉𝐈 𝐊𝐈𝐌𝐈𝐓𝐈 𝐀𝐓𝐎𝐀 𝐖𝐈𝐓𝐎 𝐊𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀 𝐊𝐔𝐎𝐌𝐁𝐄𝐀 𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Monday, July 6, 2026

𝐌𝐂𝐇𝐔𝐍𝐆𝐀𝐉𝐈 𝐊𝐈𝐌𝐈𝐓𝐈 𝐀𝐓𝐎𝐀 𝐖𝐈𝐓𝐎 𝐊𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀 𝐊𝐔𝐎𝐌𝐁𝐄𝐀 𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀

 Mchungaji William Kimiti akihubiri

......................................

MCHUNGAJI wa Kanisa la 'Redemption Evengelistic Church (REC)', Madhabahu ya Uzima, William Kimiti, ametoa wito kwa Watanzania  kuomba daima ili  kusitokee vurugu nchini.


Wito huo alitoa katika ibada iliyofanyika jana, Julai 5, mwaka huu, kwenye kanisa hilo, lililoko Kinyamwezi, Pugu, Ilala jijini Dar es Salaam. 


Mchungaji Kimiti alisema kuwa kipindi hiki, Taifa linakabiliwa na taharuki kubwa ya vijana kudai maandamano, hivyo watanzania wanatakiwa kusali ili kusitegemee nguvu ya mwilini. 


"Nitoe wito kwa watanzania, tuombe sana ili kuondoa taharuki, tusitegemee nguvu ya mwilini," alisema Mchungaji Kimiti.

 

Alisema kuwa mara zote injili inasema vita haipigani mwilini, bali ni kumuomba mwenyezi Mungu.                                

Katika mahubiri yake, Mchungaji Kimiti alitoa ujumbe kwa waumini  juu ya wito wa Mungu.               

                   

Mchungaji Kimiti alisema kwamba huwezi kuwa kwenye wito wa Mungu, wakati una dhambi, huku akinukuu neno la Mungu kutoka kitabu cha Luka sura ya 10:41_42.


Alisema kuwa ujumbe mzuri kuzungumzia ni watu juu ya wito, kwani adui amekuwa akichukua wito wa Mungu.  


Katika mahubiri yake, Mchungaji Kimiti alitaja sababu sita ambazo zinaweza kusababisha kupoteza wito wa Mungu.


Mchungaji Kimiti alisema kuwa kuna mifano mingi katika maandiko, hivyo kila mtu anatakiwa kujitafakari ndani ya nafsi yake kuhusu kumkiri kristo ili aokoke. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad