.....................................
Na Onesmo Kapinga.
MKOA wa Pwani unatarajia kuandaa maonyesho ya tano ya uwekezaji yaliyopanngwa kufanyika Oktoba 5, mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Afisa Uwekezaji Biashara na Viwanda wa mkoa huo, Rehema Akida Mchumi, wakati akiongea na waandishi wa habari jana, Julai 6, 2026, kwenye Maonyesho ya 50 ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Pwani ambao wana banda lao la maonyesho ya viwanda, Mchumi alisema kuwa Mkoa wa Pwani una fursa nyingi za biashara, ambapo alitoa wito kwa wawekezaji kwenda kuwekeza.
Alisema kuwa ujenzi wa viwanda umeongeza thamani ya mazao ya kilimo kama korosho, Nazi, ufuta, mihogo na mengine.
Afisa huyo alisema kuwa matunda kama matikiti, mananasi, ndizi, machungwa pia yameongeza thamani ya mazao ya kilimo.
Pia lisema kuwa usindikaji wa maziwa, kumeongeza thamani ya ngozi, utengenezaji wa saruji, vyakula na mifungo.
Mchumi alisema kuwa kuwapo kwa machinjio ya kisasa, vifungashio, kuchakata mazao yanatokana na misitu, samani na magogo na uchakataji wa chumvi kumeongeza thamani ya mazao hayo.
Alisema kuwa Mkoa wa Pwani kumekuwa na miundombinu, ujenzi wa nyumba za kuishi, ofisi, masoko ya kisasa, maduka makubwa, maghala, viwanja vya michezo, dampo, vituo vya mabasi na maegesho.
Mchumi alisema kuwa mkoa wa Pwani kumekuwa na fursa nyingine za kibiashara kama ujenzi wa mitambo ya kisasa ya kuchakata mawe, uchimbaji kumeongeza thamani ya madini ya dhahabu.
Kwa upande wa utalii alisema kuwa hoteli, majumba ya starehe, kumbi za mikutano, vivutio vya michezo na miundombinu mingine imejengwa.
Mchumi aliwakaribisha wafanyabiashara wadogo na wakubwa kwenda kufanya uwekezaji katika mkoa huo, kwani fursa ni nyingi.










No comments:
Post a Comment