𝐁𝐀𝐋𝐎𝐙𝐈 𝐊𝐀𝐆𝐀𝐍𝐃𝐀 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐇𝐀𝐓𝐈 𝐙𝐀 𝐔𝐓𝐀𝐌𝐁𝐔𝐋𝐈𝐒𝐇𝐎 𝐊𝐖𝐀 𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐔𝐑𝐈𝐓𝐈𝐔𝐒. - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Tuesday, July 7, 2026

𝐁𝐀𝐋𝐎𝐙𝐈 𝐊𝐀𝐆𝐀𝐍𝐃𝐀 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐇𝐀𝐓𝐈 𝐙𝐀 𝐔𝐓𝐀𝐌𝐁𝐔𝐋𝐈𝐒𝐇𝐎 𝐊𝐖𝐀 𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐔𝐑𝐈𝐓𝐈𝐔𝐒.

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Mauritius, Kamishna wa Polisi (CP) Suzan Kaganda, mwenye makazi yake ya kikazi Jijini Harare, Zimbabwe, amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Mauritius, Mhe. Dharambeer Gokhool, katika hafla iliyofanyika Julai 6, 2026, Ikulu ya Serikali iliyopo Reduit, Mauritius.


Baada ya kuwasilisha hati hizo, Balozi Kaganda alifanya mazungumzo na Mheshimiwa Rais Gokhool, ambaye alimpongeza kwa uteuzi wake na kumkaribisha rasmi katika eneo lake la uwakilishi, huku Rais huyo pia akimhakikishia ushirikiano na Serikali ya Mauritius katika kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu yake ya kidiplomasia.

Kwa upande wake, Balozi Kaganda alishukuru kwa mapokezi mazuri aliyopatiwa na kuahidi kuendeleza ushirikiano wa karibu na Serikali ya Mauritius katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Mauritius ambapo aliweka wazi kuwa dhamira yake ni kuendeleza ushirikiano katika sekta za biashara, uwekezaji, utalii na Uchumi wa Buluu kwa manufaa ya wananchi na maendeleo ya nchi hizo mbili.

Balozi (CP) Kaganda pia anaiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Zimbabwe, akiwa na makazi ya kikazi jijini Harare.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad