Kulea mtoto kwa maadili mema na kumpa kila hitaji la msingi ni ndoto na furaha ya kila mzazi, lakini pale mwanao anapogeuka kuwa janga la familia, ukaidi unapotawala, na anapojiunga na magenge ya uhalifu na matumizi ya dawa za kulevya, maisha ya wazazi hugeuka kuwa msiba wa kila siku.
Kwa zaidi ya miaka mitatu, mwanangu wa kiume aliyekuwa mwenye nidhamu na aliyefanya vizuri shuleni alibadilika ghafla. Alianza kutoroka shule, kuvuta bangi, na hatimaye kujiunga na kundi la vijana wa mtaani waliokuwa wakifanya wizi na kuwapiga watu nondo usiku.










No comments:
Post a Comment