Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolph Mkenda (wa pili kulia), akipata maelezo kutoka kwa Mwanafunzi Jackline Habibu Ndee (kushoto), ambaye anajifunza masomo Amali alipotembelea banda la shule za Sekondari kabla ya kufungua Maonesho ya Wiki ya Taifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2026, yanayofanyika katika Viwanja vya Usagara, Jijini Tanga Agosti 18, 2026.
.............................
Na Dotto Mwaibale, Tanga
WAZIRI wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolph Mkenda amesema Rais wa Jamhuri ya
Muungamo wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassani ni kiongozi wa vitendo na siyo
maneno.
Profesa
Mkenda ameyasema hayo wakati akifungua Maonesho ya Wiki ya Taifa ya Elimu,
Ujuzi na Ubunifu 2026, yanayofanyika katika Viwanja vya Usagara, Jijini Tanga Agosti
18, 2026.
“Rais Samia katika kuendeleza maendeleo utaona kazi kubwa aliyoifanya ya kasi ya Teknolojia nchini kufikia kwenye muelekeo mzuri wa kutuwezesha kufanya shughuli zetu wenyewe badala ya kutegemea wataalamu kutoka nje,” alisema Profesa Mkenda.
Alisema kwa
maelekezo ya Rais Samia hakuna haja tena ya wageni kufanya kazi kwa gharama kubwa
bali zitafanywa na Watanzania.
Profesa
Mkenda aliongeza kuwa katika kukamilisha jambo hilo aliagiza zijengwe sekondari
za wasichana kwa ajili ya masomo ya
sayansi kila mkoa ambapo baadhi zilizokamilika tayari amezizindua.
Profesa Mkenda
alisema lengo la Rais ni kuhakikisha tunaongeza uwezo wa kisayansi kwa wanafunzi na pili kupewa nafasi ya kwenda
kusoma nje ya nchi.
“ Rais Samia aliagiza kuwa ili kuwavutia wanafunzi wenye uwezo na vipaji vikubwa kusoma sayansi, hisibati, Tehama, Uhandisi na elimu tiba watapata ufadhili wa Serikali kwa asilimia 100,” alisema Profesa Mkenda.
Alisema
serikali inatoa ufadhili huo kwa wanafunzi waliofanya vizuri kidato cha sita ambapo
watapewa fedha za kujikimu, kulipia ada, vifaa vya shule mpaka watakapo maliza
masomo yao kupitia utaratibu uliowekwa.









No comments:
Post a Comment