𝐁𝐀𝐑𝐑𝐈𝐂𝐊 𝐘𝐀𝐑𝐈𝐃𝐇𝐈𝐒𝐇𝐖𝐀 𝐍𝐀 𝐇𝐔𝐃𝐔𝐌𝐀 𝐙𝐀 𝐊𝐎𝐃𝐈 𝐙𝐀 𝐓𝐑𝐀, 𝐘𝐚𝐒𝐈𝐅𝐔 𝐌𝐀𝐙𝐈𝐍𝐆𝐈𝐑𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐊𝐈𝐒𝐇𝐈 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Friday, September 4, 2026

𝐁𝐀𝐑𝐑𝐈𝐂𝐊 𝐘𝐀𝐑𝐈𝐃𝐇𝐈𝐒𝐇𝐖𝐀 𝐍𝐀 𝐇𝐔𝐃𝐔𝐌𝐀 𝐙𝐀 𝐊𝐎𝐃𝐈 𝐙𝐀 𝐓𝐑𝐀, 𝐘𝐚𝐒𝐈𝐅𝐔 𝐌𝐀𝐙𝐈𝐍𝐆𝐈𝐑𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐊𝐈𝐒𝐇𝐈

KAMPUNI ya Uchimbaji Madini ya Barrick imeeleza kuridhishwa na huduma za kodi zinazotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kusifu mazingira ya kodi ambayo ni shirikishi kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja Mkazi wa Barrick Gold Mine Tanzania  Melkiory Ngido wakati wa kikao baina ya Uongozi wa Kampuni hiyo na Kamishna Mkuu wa TRA Yusuph Juma Mwenda katika ofisi za TRA jijini Dar es Salaam. 


Ngido amesema utaratibu uliowekwa na TRA wa kufungua milango na kukutana na Walipakodi kujadili masuala mbalimbali ya kikodi umekuwa na tija katika kuongeza uelewa wa kodi na kuhamasisha ulipaji wa kodi kwa hiari. 


"Sisi tumekuwa na utaratibu wa kila mwaka kukutana na Uongozi wa TRA kueleza hali yetu ya kibiashara na namna tutakavyolipa kodi, na kama ambavyo imekuwa kwa vipindi vingine hali yetu kibiashara ni nzuri na tutaendelea kulipa kodi kwa hiari" amesema Ngido. 


Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa TRA Yusuph Juma Mwenda amesema Mamlaka hiyo itaendelea kuboresha huduma zake kwa walipakodi, kutoa elimu ya kodi na kuwezesha biashara. 


Amesema TRA inatambua na kuthamini mchango wa Kodi wa Barrick Gold Mine wakiwa ni walipakodi wakubwa pamoja na walipakodi wengine kote nchini na kuwa milango ya taasisi hiyo ya Umma ipo wazi kwaajili ya kuwasikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili walipakodi kote nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad