Na Sixmund Begashe, Moshi
WAKAZi wa Mkoa wa Kilimanjaro na viunga vyake wameendelea kupata burudani ya kipekee kutoka kwa timu yao ya Maliasili ya Mpira wa Pete Wanawake katika michuano ya SHIMIWI 2026, inayoendelea mjini hapa.
Wakazi hao mara hii wameshuhudia timu hiyo ya Wizara ya Maliasili na Utalii ikiibuka na ushindi mnono wa magoli 41-14 dhidi ya wapinzani wao timu ya RAS Lindi, huku wakieleza kuwa hawajawahi kujuta kuzishangilia timu zote za Maliasili Sports Club kwa kuwa zinawapa zaidi ya burudani.
Shabiki kindakindaki wa timu za Malisili aliyejitambulisha kwa jina la Mama Tairo mkazi wa Rombo, amesema sababu ya kuzishabikia timu hizo ni kutokana na manufaa makubwa wanayopata kutokana na uhifadhi wa Mlima Kilimanjaro.
Mwalimu wa timu hiyo yenye wachezaji mahiri na machachari
Bi. Rehema Kapela amesema siri ya ushindi wao ni kutokana na nidhanu ya wachezaji wake na kujituma.
Naye Nahodha wa timu hiyo Bi. Rachel Mkanza ameushukuru uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuendelea kuiunga mkono timu yao jambo linalowapa ari kubwa kwenye michezo yao.










No comments:
Post a Comment