Rajabu alitoa shukrani hizo Septemba 26, 2026, wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika jijini Tanga, kabla ya kumkaribisha Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, kuzungumza wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili ya kikazi mkoani Tanga.
Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi.
“Nitoe shukrani nyingi kwa Rais wetu kwa kutupatia fedha nyingi za miradi ya maendeleo. Tunasema asante sana,” alisema Rajabu.
Alisema uwekezaji unaofanywa na Serikali katika miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo umeendelea kuchochea shughuli za kiuchumi na kuvutia wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi.
Mwenyekiti huyo alitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni mradi mkubwa wa maji unaotekelezwa katika Wilaya ya Handeni, ambao ukikamilika utasaidia kumaliza changamoto ya upatikanaji wa maji iliyodumu kwa muda mrefu.
Alisema mradi mwingine ni ujenzi wa barabara zinazounganisha Mkoa wa Tanga na mikoa mingine, ikiwemo barabara ya Tanga–Bagamoyo na Tanga–Singida, zinazojengwa kwa kiwango cha lami.
“Rais ametuletea miradi mingi ndani ya Mkoa wetu wa Tanga na yenye tija kubwa kwa wananchi,” alisema Rajabu.
Habari hii imeandikwa na Dotto Mwaibale simu namba 0754362990









No comments:
Post a Comment