SHANGWE LAIBUKA BAADA YA MWENYEKITI CCM TANGA KUWAKARISHA VIONGOZI JUANI - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Monday, September 21, 2026

SHANGWE LAIBUKA BAADA YA MWENYEKITI CCM TANGA KUWAKARISHA VIONGOZI JUANI

 Aagiza viongozi kukaa pamoja na wananchi

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (MCC), Rajabu Abdulrahaman Abdallah, akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Mkata Mashariki, Wilaya ya Handeni DC, Mkoa wa Tanga Septemba 20, 2026.

..........................................

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (MCC), Ustadhi Rajabu Abdulrahaman Abdallah, amewaagiza viongozi wa CCM mkoani humo kuacha kutumia maeneo yenye kivuli wakati wananchi wanakaa juani kwenye mikutano ya hadhara.

Agizo hilo alilitoa wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Mkata Mashariki, Wilaya ya Handeni, Mkoa wa Tanga.

Abdallah alifikia hatua hiyo baada ya kukuta wananchi wamekaa juani, huku viongozi wakiwa wametengewa jukwaa lenye kivuli.

Mwenyekiti huyo aliagiza viti vipangwe juani, walikokuwa wamekaa wananchi, na kuwaagiza viongozi aliokuwa ameambatana nao kukaa pamoja na wananchi.

“Sijafurahishwa kuona tumetengewa jukwaa lenye kivuli huku wananchi wakiwa wamekaa kwenye jua, ndipo nilipoagiza vikapangwe viti juani walipokaa wananchi tukakae nao ili kama jua tulipate wote na hata kama mvua iwe hivyohivyo,” alisema Abdallah. Kauli hiyo ilizua shangwe kubwa kutoka kwa wananchi.

“Naagiza kuanzia leo sitapenda kuona viongozi wakiwa wametengewa eneo lenye kivuli wakati wa mikutano mbalimbali ya hadhara na wananchi wamekarishwa juani,” alisema Abdallah.

Viongozi wakiwa wamekaa juani na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (MCC), Rajabu Abdulrahaman Abdallah (kulia mwenye balaghashia0

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga, Mwanaisha Ulenge, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Tanga, Ramadhani Omary katika mkutano huo bila ya kujali jua kama walivyohamasishwa na Mwenyekiti waa CCM wa mkoa huo.
Wanawake wa UWT wakifanya shangwe kubwa wakiwa kwenye jukwaa walilokuwa waketi viongozi baada ya kuambiwa na Mwenyekiti CCM Mkoa wa Tanga wakae.
Wananchi wakiwa juani wakiwajibika kwa shangwe.
Viongozi wakiwa wamekaa juani (katikti mwenye miwani) ni Katibu wa CCM Wilaya ya Tanga, Feruzy Bano.

Viongozi wakibadilishana mawazo huku wakiwa wamekaa juani.

.............................................

Habari hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale Simu namba 0754362990.

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad