.............................
Na Claudia Kayombo
KUNA dhana hasa katika kizazi cha sasa kuwa tiba asili imepitwa na wakati.
Hivyo, jamiii imepunguza imani kubwa dhidi ya tiba asili na hivyo kukumbatia tiba ya kisasa.
Kimsingi kutumia tiba ya kisasa si dhambi bali tabibu wa tiba asili Japhet Ngamba maarufu kama Ngosha, anayeendesha tiba zake Chanika
Tabibu Japhet Ngamba ambaye pamoja na kutibu tiba nyingine anauwezo kumfanya yeyote aliyevunjika mifupa iwe ya miguu, mikono au hata mgongo kuunga kwa muda wa wiki mbili na baada ya hapo anaendelea kupata tiba ya kuimarisha mifupa husika.
Ngamba anasema hata ikiwa mgonjwa kiungo chake kimesagika anaweza kukiponya.
"Kuna mtu alikuja hapa amevunjika mgongo mara tatu, alikwenda hospitali ilishindikana, hapa mimi nimemtibu.
"Naomba hata watani zangu wamakonde ambao wanafanya kazi ya upasuaji wakaangukiwa na mti hadi kuwa kusagika, waje hapa mguu au mkono wao utarudi katika hali yake kama awali baada ya tiba zangu", anasema tabibu Ngamba.
Anasema kipaji cha kutibu alichonacho amepewa na Mungu kwani anasema hatumii tunguli wala manyanga ila tiba za magonjwa mbalimbali yakuwamo yasiyotibika hospitali anapoelezwa tatizo la mgonjwa dhamiri inamwambia kuwa tiba furani inafaa kwa mgonjwa husika akienda kuleta dawa husika anapona.
Hata hivyo, Ngamba anatanabahisha kuwa hali ya ajali za pikipiki ni mbaya kwani kuwa wakati anaweza kupata wagonjwa hadi 30 waliovunjika kwa ajali ya pikipiki.
Anasema si hao tu, anawatibu hata wanaosumbuliwa na kiharusi, tezi dume, kinamama wenye kizazi pingamizi na magonjwa mengine.
Anasema tiba asili hapa nchini si ngeni kwani ilianza tangu enzi za mababu ambapo magonjwa mengi yalitibiwa kwa tiba asili.
Anasema wachache wasio waaminifu ambao wamekuwa wakifanga udanganyifu katika tiba hiyo hivyo kuifanya dhalili, lakini tiba asili ina nguvu na inaweza kufanya maajabu kwa wengi hasa waliokata tamaa.
Anasema hata kwa wanaosumbuliwa na saratani nao ataweza kuwapa tiba hasa wale ambao hawajachomwa mipnzi.
Salum Abdallah mkazi wa Chanika kwa Ngwale anasema alipata ajali ya pikipiki Juni 19, mwaka huu, na alivunjika mguu, alikwenda katika hospitali mbalimbali lakini hakupata nafuu.
Hadi wiki iliyopita alipokwenda katika kituo cha tiba asili cha Ngosha sasa anaendelea vizuri.
"Maumivu makali niliyokuwa nayaona katika kipindi cha miezi mitatu yamepungua sana tangu nije hapa kupata matibabu", alisema Abdallah.
Aliendelea kubainisha, "sasa naweza kusema naendelea vizuri.
Khamis Dady 53, mkazi wa Kigogo Fresh , Dar es Sslaam, anasema alipata ajali huko Kwala Mlandizi baada ya kuanguka kutoka kwebye gari alipokuwa akishusha mabomba kwa ajili ya kuyalaza katika mitaro.
Anasema yeye alikuwa akifanya kazi kama kibarua, baada ya kuanguka alivunjika mkono na nyonga yake kuachia.
"Nilipelekwa hospitali ya wilaya, wakasema nihamishiwe Muhimbili, lakini nikashauriwa nije hapa, sasa naendelea vizuri na naamini baada ya wiki mbili nitakuwa natembea kabisa, kwani juzi nilipoletwa nilibebwa, leo nakwenda mwenyewe chooni kwa kushikilia katika ukuta", anasema.
Ngabu anasema kituo chake cha tiba maarufu kama NGOSHA kipo Chanika eneo la Kimwani maarufu kama 'Barakoa'.
Kama utahitaji kujua zaidi kuhusu tiba inayotolewa na Mtaalamu huyo unaweza kuwasiliana naye kwa kumpigia namba 0767333970.
...................................
Makala hii imeandikwa na Claudia Kayombo Namba ya Simu ni 0713144299.










No comments:
Post a Comment