Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb), akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Profesa William Pallangyoalipofika chuoni hapo kwa ajili ya mahafali ya ishirini na nne (24) ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida, yaliyofanyika Novemba 13, 2026 katika viwanja vya TIA, mkoani Singida.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb), akiongozana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Profesa William Pallangyo ( kulia) alipofika chuoni hapo kwa ajili ya mahafali ya ishirini na nne 24 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida, yaliyofanyika Novemba 13, 2026 katika viwanja vya TIA, mkoani Singida.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb), akisalimiana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Kampasi ya Singida, Dkt.James Mrema,alipofika chuoni hapo kwa ajili ya mahafali ya ishirini na nne 24 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida, yaliyofanyika Novemba 13, 2026 katika viwanja vya TIA, mkoani Singida.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb), akisalimiana na Mjumbe wa Bodi. Renetus Msangiraalipofika chuoni hapo kwa ajili ya mahafali ya ishirini na nne 24 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida, yaliyofanyika Novemba 13, 2026 katika viwanja vya TIA, mkoani Singida.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb), akisalimiana na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri Profesa Momole Kasambalaalipofika chuoni hapo kwa ajili ya mahafali ya ishirini na nne 24 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida, yaliyofanyika Novemba 13, 2026 katika viwanja vya TIA, mkoani Singida.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb), akisalimiana na Naibu Mkuu wa Chuo, Mipango, Fedha na Utawala, TIA, Dkt. Issaya Hassanalalipofika chuoni hapo kwa ajili ya mahafali ya ishirini na nne 24 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida, yaliyofanyika Novemba 13, 2026 katika viwanja vya TIA, mkoani Singida.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb), akisaini kitabu cha wageni alipofika chuoni hapo kwa ajili ya mahafali ya ishirini na nne 24 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida, yaliyofanyika Novemba 13, 2026 katika viwanja vya TIA, mkoani Singida.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius
Luswetula (Mb), akitembelea Mradi wa ujenzi wa jengo la taaluma kujionea
hatua iliyofikiwa katika ujenzi, alipofika chuoni hapo kwa ajili ya mahafali ya
ishirini na nne 24 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida,
yaliyofanyikaNovemba 13, 2026 katika viwanja vya TIA, mkoani Singida.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent
Deogratius Luswetula (Mb), akitembelea maonesho ya shughuli za ujasiriamali
zinazotekelezwa na wanafunzi, alipofika chuoni hapo kwa ajili ya mahafali ya
ishirini na nne 24 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida,
yaliyofanyika Novemba 13, 2026 katika viwanja vya TIA, mkoani Singida.
Wahadhiri wa Taasisi hiyo wakielekea kuanza maandano na wahitimu wakati wa mahafali hayo
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb), (Katikati), akiongoza maandamano ya mahafali ya ishirini na nne 24 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida katika viwanja vya TIA, Mkoani Singida. kushoto ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara, Taasisi ya Uhasibu Tanzania Ndugu William Makoresho na kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Prof. William Pallangyo.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius
Luswetula (Mb), akizungumza katika Mahafali ya Ishirini na Nne 24 ya Taasisi ya
Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida, yaliyofanyika Novemba 13, 2026 katika viwanja vya TIA, mkoani Singida.
------------------------
👇ANGALIA VIDEO HAPA
---------------------------
Serikali imesema itaendelea kuimarisha
sekta ya elimu nchini kwa kuhakikisha kila mtoto anasoma kwa miaka kumi katika
shule za Serikali bila kulipa ada, sambamba na kuimarisha elimu ya amali ili
kuwajengea vijana ujuzi wa kujiajiri na kushiriki kikamilifu katika maendeleo
ya Taifa.
Hayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa
Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb), wakati akizungumza katika
mahafali ya ishirini na nne 24 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya
Singida, yaliyofanyika Novemba 13, 2026 katika viwanja vya TIA, mkoani humo.
Luswetula alisema hatua hiyo
inalenga kuhakikisha kila kijana anahitimu akiwa na maarifa na ujuzi
utakaomwezesha kuendelea na elimu ya juu, kupata ajira au kujiajiri.
‘‘Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka
2014, Toleo la 2023, imeweka msingi wa mageuzi ya elimu yanayolenga kuandaa
wahitimu wenye uwezo wa kukabiliana na mahitaji ya soko la ajira na kuchangia
kufikia uchumi wa kipato cha kati cha juu’’, alisema
Alisema katika hatua ya elimu ya juu,
Serikali imeweka mikakati mitatu muhimu inayohusisha maboresho ya mitaala ili
iendane na mahitaji ya soko la ajira, uwekezaji katika miundombinu ya
kufundishia na kujifunzia pamoja na matumizi ya teknolojia ya habari na
mawasiliano (TEHAMA) katika ufundishaji, tafiti na utoaji wa huduma.
Luswetula alisema Mradi wa Elimu
ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) ni mfano wa uwekezaji unaolenga kuboresha
mazingira ya vyuo vikuu, ikiwemo Kampasi ya Singida.
Luswetula aliwapongeza
vijana wanaotumia teknolojia kimkakati kubuni fursa za maendeleo, ikiwemo
vijana wa TIA kampasi ya Singida walioshiriki na kushinda mashindano ya mawazo
ya biashara na kupata nafasi za kwenda kujifunza na kushindana katika nchi za
Uganda, Kenya, Afrika Kusini na Urusi .
‘‘ Mafanikio ya vijana hao yanaakisi
matarajio ya Dira 2050, inayolenga kujenga Taifa lenye vijana wenye maarifa,
ujuzi na uwezo wa kujiajiri. Kwa mujibu wa mwelekeo huo, elimu inapaswa kuwa
nyenzo ya kuwawezesha vijana kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao na
kushiriki katika kujenga uchumi imara na shindani’’, alisema
Aliwaasa wahitimu kutumia teknolojia
kwa ajili ya kutengeneza kipato, kukuza biashara na kuwafikia wateja badala ya
kuitumia katika udanganyifu, utapeli na kusambaza taarifa za uongo.
‘‘Pia, ninawahimiza kuzingatia
uwajibikaji katika taaluma zenu, kulipa kodi kwa hiari na kudai risiti halali
mnapofanya manunuzi, mkitambua mchango wa kodi katika kugharamia huduma za
maendeleo nchini,’’alisisitiza
Aidha, aliwahimiza wahitimu
walionufaika na mikopo ya elimu ya juu kuanza kurejesha mikopo wanapoanza
kupata kipato ili kuwawezesha Watanzania wengine kupata fursa ya elimu ya juu
nchini.
Luswetula alitoa rai kwa wahitimu
kutumia maarifa na ujuzi walioupata kuanzisha miradi itakayowawezesha kujipatia
kipato na kuchangia maendeleo ya jamii zao ikiwa ni pamoja na kutumia fursa za
kiuchumi zilizopo katika Mkoa wa Singida kuanzisha shughuli za uzalishaji mali
kutokana na fursa zilizopo katika kilimo cha alizeti, ufugaji, biashara na
madini.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya
Uhasibu Tanzania (TIA), Profesa William Pallangyo, akizungumza wakati
akitoa taarifa ya maendeleo ya chuo, katika mahafali ya ishirini na nne 24 ya
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida, yaliyofanyika katika
viwanja vya TIA, mkoani Singida.
👇ANGALIA VIDEO HAPA
---------------------------
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya
Uhasibu Tanzania (TIA), Profesa William Pallangyo, alisema Kampasi ya Taasisi
ya Uhasibu Tanzania (TIA) Singida wahitimu 1,656, wakiwemo wanawake 855
(asilimia 51.6) na wanaume 801 (asilimia 48.4) wametunukiwa ngazi mbalimbali na
kipekee imeweka rekodi ya kwanza ya kuhusisha wahitimu wa shahada ya uzamili tangu
kuanzishwa kwa kampasi hiyo mwaka 1974.
Alisema mafanikio makubwa yameendelea
kushuhudiwa katika uandikishaji wa wanafunzi wapya kwa mwaka wa masomo
2026/2027, ambapo tayari wanafunzi 1,631 wamesajiliwa huku idadi hiyo
ikitarajiwa kufikia 1,750, ikichangiwa na ongezeko la wanufaika wa mikopo
ya elimu ya juu ambapo wanafunzi 893 wa kampasi hiyo wamefanikiwa kupata zaidi
ya shilingi milioni 696.
‘‘Katika kuboresha mazingira ya
kujifunzia, Serikali ya Awamu ya Sita imefanya uwekezaji mkubwa wa kimkakati
kupitia mradi wa HEET chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo
ujenzi wa jengo jipya la taaluma umefikia asilimia 92 ambapo gharama ya mradi
ni sh. bilioni 13.56, hivyo utakapokamilika utaongeza uwezo wa kampasi
kuhudumia hadi wanafunzi 22,000 kutoka 2,600 wa sasa, huku ikitoa ajira za muda
mfupi kwa wananchi 600 wa mkoani hapa,’’alisema Profesa Pallangyo.
Alisema mbali na taaluma, TIA Singida
imejikita katika kutatua changamoto za kijamii kupitia tafiti 13 zilizofanywa
ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa mkoa pamoja na kutoa mchango kwa jamii
kupitia mkakati wa kuboresha ufaulu wa somo la hisabati katika Shule ya
Sekondari Mandewa, pamoja na ushiriki thabiti katika shughuli za michezo
na maendeleo ya jamii.
Profesa Pallangyo alisema mafanikio
hayo ni utekelezaji wa Dira 2050, inayosisitiza udahili wenye ubora unaoendana
na soko la ajira, wahitimu wenye ujuzi wa vitendo na uwezo wa kujiajiri, pamoja
na miundombinu ya kisasa ya kufundishia na kujifunzia.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara , Taasisi ya Uhasibu Tanzania Ndugu William Makoresho, akizungumza wakati akimkaribisha mgeni rasmi kufungua mahafali ya ishirini na nne 24 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida, yaliyofanyika Novemba 13, 2026 katika viwanja vya TIA, mkoani Singida.
Naye Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi
ya Ushauri ya Wizara , Taasisi ya Uhasibu Tanzania Bw. William Makoresho,
aliishukuru Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. Samia
Suluhu Hassan, kupitia Wizara ya Fedha, kwa kuendelea kuikuza TIA, na kuahidi
kuwa Bodi itaendelea kuishauri menejimenti, ili kuhakikisha TIA inaendelea
kutekeleza majukumu yake kikamilifu.
Aliwaasa wahitimu kujenga uwezo wa
kiuchumi kwa kujifunza kutunza na kuendesha fedha, kujiwekea akiba,
kufanya maamuzi ya busara kuhusu fedha pamoja na kuziona fursa za uzalishaji na
uwekezaji zinazowazunguka ili kujenga msingi thabiti wa maisha ya
baadaye.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhasibu
Tanzania Kampasi ya Singida, Dkt.James Mrema, akizungumza katika mahafali ya
ishirini na nne 24 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida,
yaliyofanyika Novemba 13, 2026 katika viwanja vya TIA, mkoani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhe. Godwin Gondwe,
akizungumza na wahitimu katika Mahafali ya Ishirini na nne 24 ya Taasisi ya
Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida katika viwanja vya TIA, mkoani
Singida.
Mshereheshaji (MC) wa mahafali hayo, Imani Matonya akiwajibika.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius
Luswetula (Mb), akiwatunuku ngazi mbalimbali ya cheti wahitimu katika mahafali
ya ishirini na nne 24 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida
katika viwanja vya TIA, mkoani Singida.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb), akiwatunuku ngazi mbalimbali ya cheti wahitimu katika mahafali ya ishirini na nne 24 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida katika viwanja vya TIA, mkoani Singida.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius
Luswetula (Mb), akimkabidhi zawadi mhitimu wa shahada ya pili ya uhasibu
aliyefanya vizuri, Diana Kisaka, katika mahafali ya ishirini na nne 24 ya Taasisi
ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida, yaliyofanyika katika viwanja vya
TIA, mkoani Singida.
Kushoto ni Mshereheshaji ( MC ) wa mahafali hayo, Imani Matonya, MC Daudi Mashauri ( katikati )Naibu Mkuu wa Chuo, Mipango, Fedha na Utawala, TIA, Dkt. Issaya Hassanal wakiwa katika mahafali hayo.
Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo
Ndugu ,Jamaa, Marafiki na Wazazi wa Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mahafali yakiendelea
Ndugu ,Jamaa, Marafiki na Wazazi wa Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo
Wahadhiri wa Chuo hicho wakiwa kwenye mahafali hayo.
Viongozi wa TIA wakiwa kwenye mahafali hayo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Profesa William Pallangyo, akizungumza.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Profesa William Pallangyo, akiwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma,, Utafiti na Ushauri Profesa Momole Kasambala ( katika ), Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Kampasi ya Singida, Dkt.James Mrema, wakati wa mahafali hayo.
Picha ya pamoja
--------------------------------------
TAZAMA VIBE LA WAHITIMU! SHANGWE, FURAHA NA NDEREMO KATIKA MAHAFALI YA 24 TIA SINGIDA.
--------------------
(Habari / picha imeandaliwa na mtandao wa Singidani Blog)
No comments:
Post a Comment