Marafiki wa Watoto wa Kiume wa Marehemu Mzee Alinanine Mafumu Mlagha wakiwa wamebeba jeneza wakati wakitoka Chumba cha Kuhifadhia Maiti Hospitali ya Wilaya ya Makandana Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya Novemba 10, 2026.
.............
Na Dotto
Mwaibale, Mbeya
MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God Tanzania (EAGT), lililopo Kitongoji cha Newland, Kijiji cha Ibula, Kata ya Kiwira, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya, Keneth Kabefu, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kuruhusu shughuli za kidini kufanyika nchini kwa uhuru na amani.
Kabefu alitoa pongezi hizo Novemba 10, 2026, wakati akiongoza ibada ya mazishi ya Mzee Alinanine Mafumu Mlagha (84), mkazi wa kitongoji hicho, aliyefariki dunia Novemba 7, 2026, kutokana na ugonjwa wa saratani ya koho.
“Sisi kama kanisa tunampongeza na kumshukuru Rais Samia kwa kuruhusu shughuli za kidini kufanyika nchini kwa uhuru na amani, tofauti na hali ilivyo katika baadhi ya nchi duniani,” alisema Kabefu.
Aidha, aliipongeza Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia kwa kudumisha amani nchini, hali inayowawezesha waumini wa dini mbalimbali kuendelea kuabudu kwa uhuru bila kubughudhiwa.
Akihubiri katika ibada hiyo na kunukuu kitabu cha Mathayo, Mchungaji Kabefu alisema Mkristo anapaswa kuwa msafi wa kiroho wakati wote badala ya kujikita katika kupendezesha mwili pekee.
“Leo hii tunaona watu wanavyojenga nyumba za kisasa, kuvaa mavazi mazuri na kula vyakula vizuri. Yote hayo wanayafanya kwa ajili ya kupendezesha miili yao badala ya kusafisha mioyo yao kama Mungu anavyohitaji,” alisema.
Alitoa wito kwa wanadamu kubadilika kwa kusafisha mioyo yao kupitia Yesu Kristo badala ya kuwekeza maisha yao katika kupendezesha miili na kufuatilia mambo ya dunia.
Akizungumzia maisha ya marehemu Mzee Mafumu, Kabefu alisema kuwa wakati akiugua, alifika kanisani hapo akiomba kubatizwa. Hata hivyo, wakati wakipanga siku ya ubatizo akiwa nyumbani kwake pamoja na mke wake, alianza kuomba huku akimwomba Mungu amsamehe dhambi zake na kulia.
“Tangu alipoomba msamaha hazikupita siku nyingi kabla ya kufariki dunia. Hivyo, kiimani tunaamini amepokelewa peponi na ndiyo maana kanisa lipo hapa kwa ajili ya mazishi yake,” alisema Kabefu.
Kwa upande wake, Mchungaji Gidion Mwamboneke wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God Tanzania (EAGT), lililopo Kitongoji cha Kanyegele, aliwataka watu kujiandaa vyema kiroho kwa ajili ya mwisho wa maisha yao, akieleza kuwa hakuna anayejua siku atakayofariki dunia.
Akiongoza ibada ya mazishi, Mwamboneke alisema kuwa kila mwanadamu anapaswa kumtambua Mungu aliyemuumba, iwe anapitia nyakati za mafanikio au changamoto za maisha.
Alisema
Mungu ndiye aliyewaumba wanadamu na kwamba anapaswa kupewa nafasi ya kwanza
katika maisha yao.
“Mungu ndiye aliyetufanya tuwepo hapa duniani. Si kwa ujanja wa mtu yeyote, labda kama kuna mtu anajivunia njia nyingine. Lakini kihistoria hakuna mtu mwenye umri wa miaka 150 hadi 200. Mtu akifikisha zaidi ya miaka 100, huwa habari kubwa na jambo la kushangaza,” alisema.
Aliongeza kuwa kazi ya wainjilishaji ni kuwakumbusha wanadamu wasimsahau Mungu wanapoendelea kuishi, kustawi na kupata mafanikio, kwa kuwa kifo kinaweza kuja wakati ambao hawautarajii.
Alisema wainjilishaji wanaendelea kusisitiza ujumbe huo ili kuwasaidia wanadamu kujiandaa na kufikia mwisho mwema wa maisha yao.
“Mtu yeyote aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi duniani zinahesabika. Hivyo, tuendelee kumtumikia Mungu wakati wote,” alisema Mchungaji Mwamboneke.
Mchungaji Gidion Mwamboneke akihubiri kwenye ibada hiyo.
Mchungaji Michael Mwankanye akizungumza kwenye ibada hiyo.
Taswira ya ibada hiyo
Mchungaji Mary Ikenda akiongoza kuomba wakati wa ibada hiyo.
Ndugu, jamaa na familia ya marehemu wakiwa kwenye ibada hiyo. Kulia ni mtoto wa kwanza wa marehemu, Twitikege Alinanine Mafumu Mlagha.
Mpwa wa Marehemu, Kulwa Mwaibale akisoma historia ya marehemu.
Ibada ikiendelea.
Marafiki wa watoto wa kiume wa marehemu wakiwa kwenye ibada hiyo. Kutoka kushoto ni mdogo wake Edward Kalongoti, Mr Keny na Robert Nselu.
Jeneza lenye mwili wa marehemu likishushwa kaburini
Marafiki wa watoto wa marehemu kutoka Wilaya ya Chunya na Mbeya Mjini wakiwa kwenye ibada hiyo.
Mchungaji Gidion Mwamboneke akisimika msalaba kwenye kaburi la marehemu wakati wa mazishi.
Ibada ya mazishi ikiendelea.
Wapwa wa marehemu, Mary Anyitike (kushoto) na Ambwene Kyoga wakiwa kwenye ibada hiyo
Ibada ikiendelea.
Huzuni ikutamalaki kwenye msiba huo.
Wanakwaya ya Kanisa la EAGT kutoka Kitongoji cha Kanyegele wakiimba katika msiba huo.
Familia ya marehemu wakiwa kwenye ibada hiyo. Kutoka kushoto ni Mjukuu wa Marehemu Sophia Furaha, mtoto wa marehemu Christina na Ester.
Taswira ya ibada hiyo.
Mpwa wa Marehemu, Nico Mwaibale, akimpa pole Binamu yake Furaha kwa kufiwa na baba yaake.
Wanakikundi cha Ubalozi Sogea kutoka Kitongoji cha Kanyegele wakiwa kwenye ibada hiyo.
Mwinjilisti wa Kanisa la EAGT kitongoji cha Newland Joshua Ngofyela, akimkabidhi sadaka mtoto wa marehemu Furaha Mafumu wakati wa ibada hiyo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ibula, Amos Mwaipwisi, akizungumza wakati wa ibada hiyo na kutoa salamu za serikali.
Mshereheshaji (MC) Patrick Mwambona kutoka Kampuni ya Jose Music, akiwajibika ipasavyo wakati wa ibada hiyo.
Mjukuu wa Marehemu Sophia Furaha (kushoto), akisaidiwa baada ya kuzidiwa wakati wa mazishi ya babu yake.
Muonekano wa nyumba ya milele (kaburi) la Mzee Alinanine Mafumu Mlagha.
Mchungaji Gidion Mwamboneke akiweka udongo kaburini.
Mjukuu wa marehemu Sophia Furaha, akiweka udongo kaburini ikiwa ni ishara ya kumzika babu yake.
Mpwa wa marehemu, Kulwa Mwaibale akiweka udongo kaburini ikiwa ishara ya kumzika mjomba wake.
Huzuni ikitamalaki kwenye mazishi hayo.
Mazishi yakiendelea.
Mjane wa marehemu Rejina Kyenda, akiweka shada kwenye kaburi la mume wake.
Watoto wa marehemu Fred na Furaha Mafumu, wakiweka shada kwenye kaburi la baba yao.
Mashada yakiwekwa kwenye kaburi.
Wadogo zake marehemu wakiwekwa mashada kwenye kaburi la kaka yao.
Wakamwana wa marehemu wakiweka shada kwenye kaburi
Wajukuu wa marehemu wakiweka shada.
Wapwa wa marehemu wakiweka mashada kwenye kaburi la mjomba wao. Kulia anaye shiriki kuweka shada ni Dotto Mwaibale.
Wachungaji walioshiriki mazishi hayo wakiweka mashada ya maua kwenye kabari la marehemu Alinanine Mafumu Mlagha.










No comments:
Post a Comment