MBUNGE JESCA KISHOA ALIVYOPELEKA TABASAMU KWA WANANCHI WILAYA YA MKALAMA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Tuesday, April 23, 2024

MBUNGE JESCA KISHOA ALIVYOPELEKA TABASAMU KWA WANANCHI WILAYA YA MKALAMA

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Jesca Kishoa akizungumza na Wananchi wa Kata ya Ibaga, Wilaya ya Mkalama wakati alipokuwa katika ziara yake ya kikazi wilayani humo Aprili 21, 2024. 

..........................................

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Jesca David Kishoa  Jumamosi amefanya ziara ya kikazi katika kata ya Ibaga, Wilaya ya Mkalama ambayo ilikuwa mahsusi ya kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya katika kuliongoza na kuliletea maendeleo Taifa letu. ambapo pia alitatua kero mbalimbali za wananchi kama ifuatavyo: 

1. Kugawa Mitungi ya gesi ya kupikia Kwa kinamama wajasiriamali (Mama Lishe) 30. 

2. Kugawa jezi za mpira Kwa timu 15 zinazotoka Kata ya Ibaga. 

3. Ametembelea na kuchangia kiasi cha Tshs. 3,700,000/= ili kumalizia ujenzi wa zahanati ya Ibaga. 

4. Ameviunga mkono vikundi 26 vya wanawake, wazee na vijana kwa kuviongezea akiba ya fedha kwenye shughuli zao. 

5. Pia ametatua kero ya mgonjwa aliyepata ajali katika Kijiji Cha Ibaga na kesho mgonjwa huyo ataendelea na matibabu Hospitalini. 

Aidha Mheshimiwa Mbunge amewahamasisha wananchi kudumisha mshikamano na kumuunga mkono Dkt. Samia Suluhu Hassan.Wanawake wa Kata ya Ibaga wakiwa na majiko ya gas waliyopewa na mbunge huyo

Wananchi wa Kata ya Ibaga wakimsikiliza Mbunge Kishoa alipokuwa akiwahutubia.
Mbunge Kishoa akisikiliza kero kutoka kwa mmoja wa wananchi wa kata hiyo.
Wanawake wakionesha furaha zao kwa kuonesha mabango yenye ujumbe mbalimbali kwa mbunge wao.

Mmoja wa vijana wa Kata ya Ibaga akiwa amelala barabarani akionesha furaha yake wakati wa mapokezi ya mbunge huyo alipowasili kwa ajili ya ziara hiyo.
Mbunge Kishoa akisikiliza  kero huku akiwa amembeba mtoto wa wananchi waliofika kumuona wakati wa ziara hiyo.
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad