...............................
Na Dotto Mwaibale
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Suma Fyandomo ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Kuruhusu Mikopo ya 10% kwa Walemavu, Vijana na Wanawake yaani (4,4,2) inayotolewa kupitia Halmashauri za wilaya nchini.
Fyandomo alitoa pongezi hizo hivi karibu kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi wakati wa ziara yake aliyoifanya mkoani humo ya kusikiliza kero za wananchi ili kuzitafutia ufumbuzi na kuimarisha chama..
"Mhe. Katibu Mkuu nachukua nafasi hii kutoa pongezi zangu kwa Serikali kwa niaba ya wanawake wa Mkoa wa Mbeya kwa kurudishwa kwa mikopo hiyo ambayo ilikuwa ni muhimu na msaada mkubwa kwa makundi haya tunamshukuru sana Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan," alisema Mbunge Fyandomo.
Mbunge Fyandomo alisema wanawake wa Mkoa wa Mbeya ni wachakarikaji wakubwa kwa biashara mbalimbali hivyo kurejeshwa kwa mikopo hiyo kutawaongezea ari ya kufanyabiashara zao jambo litakalo wainua kiuchumi katika familia zao na Taifa kwa ujumla.
Katika ziara hiyo iliyofanyika mikoa sita Dkt. Nchimbi aliongozana na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Amos Makalla na Katibu wa NEC Idara ya Organaizesheni, Issa Haji Ussi Gavu.










No comments:
Post a Comment