HAIDERALI GULAMALI ACHUKUA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA ILONGERO, MBUNGE ALIYEMALIZA MUDA WAKE KUMPA USHIRIKIANO - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Sunday, August 24, 2025

HAIDERALI GULAMALI ACHUKUA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA ILONGERO, MBUNGE ALIYEMALIZA MUDA WAKE KUMPA USHIRIKIANO


Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Haiderali Gulamali Mgombea aliyeteuliwa na chama hicho  kuwania ubunge Jimbo la Ilongero mkoani Singida, amechukua fomu ya kuwania nafasi hiyo katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Singida.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu, Gulamali alianza kwa kuwashukuru  wana CCM,viongozi wa chama hicho na wananchi kwa umoja wao kwa kuwekeza imani kubwa kwake kwa jinsi walivyompigia kura nyingi wakati wa mchakato wa kura za maoni zilizomfanya aibuke mshindi.

"Nawashukru wananchi na wanachama wa CCM,Kamati Kuu na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuniamini, kazi niliyoomba ni ya utumishi niwawakikishie wananchi nitawatumika kwa uaminifu mkubwa kabisa na kuhakikisha Ilongero inapiga hatua kwa kutumia ilani ya CCM ya 2025/ 2030 ambapo nitaangalia vipaumbele vya wananchi," alisema Gulamali.

Kwa upande wake mbunge aliyemaliza muda wake Ramadhan Ighondo amewashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa ushirikiano wao mkubwa waliompa kwa miaka mitano ya utumishi wake.

“Kwa pamoja tumelijenga jimbo letu kwa kuleta maendeleo na kupiga hatua kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine na uongozi ni kupokezana vijiti.

Nichukue nafasi hii kumpongeza mgombea wa CCM katika Jimbo la Ilongero kwa kipindi hiki ndugu Haiderali Gulamali na namuombea utumishi mwema wenye kuacha alama na nitashirikiana naye na Wana CCM wote kadri itakavyohitajika bila kinyongo chochote,” alisema Ighondo.

Ighondo alikishukuru Chama wilaya, mkoa na Taifa Kwa ushirikiano mkubwa waliomipa wakati wa utumishi wake na kueleza kuwa sasa kazi moja kubwa waliyo nayo ni kwenda kupiga kura nyingi za Mgombea Urais DKT Samia, wabunge wa CCM, Madiwani wa CCM kwani lengo letu ni kushika Dola....SOMA ZAID

 Haiderali Gulamali akikabidhiwa fomu

Haiderali Gulamali, akijaza fomu hizo baada ya kukabidhiwa.

Haiderali Gulamali akielekea kuchukua fomu Ofisi ya Tume Huru ya Uchaguzi wilayani humo.
Haiderali Gulamali akisoma maelekezo yaliyomo kwenye fomu hiyo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad