Mkuu wa Mkoa wa Songwe Jabir Omary Makame akizungumza na madereva bajaji, bodaboda na maguta walioshiriki Jogging iliyoandaliwa na Maafisa usafirishaji wilayani Mbozi iliyofanyika Agosti 9, 2025 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa huo.
.................................................
Na Mwandishi Wetu, Songwe.
MKUU wa Mkoa wa Songwe Jabir Makame ameyataka makundi ya waendesha pikipiki maarufu bodaboda, Bajaji, maguta, wajasiriamali wadogo wadogo kuchangamkia fursa ya mikopo ya riba nafuu inayotolewa na serikali kupitia benki ya NMB kwa wananchi.
Amesema hayo leo Jumamosi Agosti 9, 2025 wakati wa jogging iliyoandaliwa na maafisa usafirishaji wakiongozwa na madereva bajaji na na pikipiki ikiwa na lengo la kumkaribisha Mkuu huyo katika Wilaya ya Mbozi baada ya kuteuliwa Juni 23, 2025 kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe.
Amesema Serikali baada ya kuona fedha asilimia kumi zinazotolewa na Halmashauri zote nchini hazitoshi kuyanufaisha makundi yote , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan aliamua kuongeza mikopo kupitia benki ya NMB ili kuyafikia makundi yote yakiwemo ya bodaboda, Bajaji, wajasiriamali na machinga.
"Mfuko maalum wa fedha ambao umeandaliwa na Rais Samia.. changamkieni fursa fedha hizi hazina mashariti yoyote , Serikali inathamini sana kazi zenu ninyi waendesha pikipiki, Bajaj , wamachinga na wajasiriamali kwa sababu mna mchango mkubwa kuchangia mapato ya nchi yetu" amesema Makame.
Amewashukuru waendesha pikipiki na Bajaj kwa kuandaa tukio kubwa la kumkaribisha katika Wilaya ya Mbozi, tukio lililoambatana na mazoezi ya mwili (jogging) katika Mji wa Vwawa.
Aidha Mhe. Makame amewaahidi kuwapa ushirikiano mkubwa katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Akisoma Risala kwa Mkuu wa Mkoa, Katibu wa Madereva bodaboda Wilaya ya Mbozi, Abel Mwambene amesema Serikali ya Mkoa wa Songwe imekuwa na ushirikiano mzuri ambao umeimarisha na kudumisha amani .
Amesema wameandaa tukio hilo la kihistoria kumkaribisha Mkuu wa Mkoa ili kuendelea kushirikiana kutatua changamoto mbalimbali hasa magendo katika na matukio ya udokozi.
Maafisa Usafirishaji wa MMkoa wa Songwe (katikati walioshika mbuzi) wakimkabidhi kitoweo hicho mkuu wa mkoa huo Jabir Omary Makame kwa ajili ya kumpa Rais Samia Suluhu ili apate supu ikiwa ni kumpongeza baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya urais.Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Hamad Mbega akisisitiza jambo baada ya kushiriki jogging na maafisa usafirishaji wa mkoa wa Songwe.
Mazoezi mbalimbali yakifanyika wakati wa Jogging hiyo.
Mazoezi yakiendelea kufanyika.
Mazoezi yakiendelea.
Mazoezi yakiendelea. 'Hapa ni kanyaga twende'
Mazoezi yakipamba moto. Kutoka kushoto mwenye miwani ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Jabiri Omary Makame, Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Hamad Mbega na Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Nicholas Livingstone.









No comments:
Post a Comment