VIONGOZI IGENI UCHAPAKAZI WA WAZIRI HUYU - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, August 23, 2025

VIONGOZI IGENI UCHAPAKAZI WA WAZIRI HUYU

Naibu Waziri Wizara ya Sayansi na Teknolojia, Mhe. Maryprisca Winfred Mahundi

....................................... 

Na Mwandishi Wetu 

Viongozi wa Serikali hususan mawaziri wametakiwa kuiga uchapakazi wa Naibu Waziri Wizara ya Sayansi na Teknolojia, Mhe. Maryprisca Winfred Mahundi.

Wito huo umetolewa na mmoja wa wananchi aliyekuwa na changamoto ya binti yake aliyeomba namba ya NAPA kwa lengo la kupata mkopo wa elimu ya juu, mtandao ukawa hauruhusu taarifa zake kufunguka alivyomsaidia kutatua tatizo hilo kwa muda mfupi.

Mwananchi huyo ambaye ameomba kuhifadhiwa jina lake amesema jana usiku aliwasiliana na waziri huyo na kumueleza changamoto yake ambapo alimueleza kuwa atamfahamisha msaidizi wake atakayempigia simu mwananchi huyo leo hii asubuhi (Agosti 23, 2025) ili afuatilie kujua tatizo liko wapi.

"Asante kwa taarifa na pole sana kwa changamoto hiyo, ninawasiliana na msaidizi wangu, atafuatilia kujua tatizo lipo wapi halafu mapema kesho asubuhi (Leo tarehe 23) atakupigia simu," mwananchi huyo alimnukuu Waziri Mahundi.

Mwananchi huyo ameongeza kuwa mapema asubuhi alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kwa jina moja la Simon kwamba ni msaidizi wa Naibu Waziri Maryprisca aliyempa taarifa za changamoto yake akaomba amweleze.

Amesema alipomfahamisha, alimuunganisha kwa Afisa wa NAPA aliyemueleza changamoto yake.

"Nilimwambia kwamba tangu nilipoomba namba ya NAPA mapema mwezi huu kila nilipofungua mtandao kujua kama ombi langu lilikubaliwa nilijibiwa bado linashughulikiwa, nikakosa amani kwani siku zinaisha ambapo tarehe 31 saa 6 usiku zoezi hilo linafungwa," mwananchi huyo alisema.

Aliongeza kuwa baada ya kumfahamisha hivyo na kumpa namba yake ya simu na kuingia kwenye mfumo alibaini kilichosababisha hali hiyo akakiweka sawa, muda huo huo mtandao ukafunguka na binti yake aliyemtaja kwa jina moja la Diana akapata ujumbe wa hongera kwenye simu yake kuonesha amepata barua ya kuombea mkopo kupitia NAPA.

"Nimefurahi sana bila waziri huyo kunisaidia kwa upendo binti yangu angekosa fursa ya kupata mkopo wa elimu ya juu. mawaziri wengine waige uchapakazi wake wa kuwasaidia wananchi, namuomba Rais Samia kutowaacha mawaziri wa aina yake kwenye baraza lake la mawaziri baada ya uchaguzi mkuu, au kuwapa nafasi sehemu nyingine ili waendelee kuwatumikia watanzania," alisema mwananchi huyo huku akitabasamu.

Aidha, amemshukuru afisa wa NAPA aliyemtaja kwa jina moja la Amani na msaidizi wa waziri jinsi walivyoishughulikia changamoto ya mwananchi huyu kwa haraka.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad