................................................
Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
Dkt. Asha-Rose Migiro ni mwanamke wa kwanza kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), nafasi ambayo haijawahiu kushikwa na mwanamke yeyote tangu Tanzania ipate uhuru wake mwaka 1961.
Nafasi hiyo ya Dkt. Migiro imekuja
kufuatia uteuzi uliofanywa na Kikao cha
Halmashuri Kuu ya CCM (Taifa) chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Dkt. Migiro anashika nafasi
hiyo ya juu katika chama hicho akimrithi Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye
aliteuliwa kuwa mgombea mwenza wa Dkt. Samia wa nafasi ya urais kupitia chama
hicho.
Pamoja na kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM,Dkt. Migiro ana historia ya kipekee pia nchini kwani ni mwanamke wa kwanza kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa chini ya Katibu Mkuu wa umoja huo aliyestaafu Ban Ki-moon...SOMA ZAIDI










No comments:
Post a Comment