LAZARO NYALANDU ATUA KIGOMA KUSAKA KURA ZA WAGOMBEA CCM - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Friday, September 12, 2025

LAZARO NYALANDU ATUA KIGOMA KUSAKA KURA ZA WAGOMBEA CCM

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Waziri mstaafu wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akipokelewa mkoani Kigoma ambapo amekwenda kuhimiza wanananchi na wana CCM kujitokeza kwa wingi oktoba 29 kupiga kura nyingi kwa wagombea wa CCM kuanzia Mgombea wa Urais, Ubunge na Diwani.

..............................................

Na Mwandishi Wetu, Kigoma

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Waziri mstaafu wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ameingia kwa kishindo Mkoani Kigoma leo Septemba 11, 2025, amepokelewa kwa shangwe na hamasa kubwa na wanaCCM wa Wilaya ya Kasulu wakiongozwa na Katibu wa CCM Wilaya hiyo, Jenifer Chenguile.

Akiongea na wananchi waliojitokeza, Nyalandu amesisitiza umuhimu wa mshikamano ndani ya chama na jamii kwa ujumla, akieleza kuwa CCM ndicho Chama  cha kuendeleza maendeleo ya taifa kupitia sera na miradi yenye kugusa maisha ya kila Mtanzania.

Amewataka wananchi wote wenye sifa na kadi ya kupiga kura kujitokeza kwa wingi ifikapo siku ya Uchaguzi Mkuu wa 2025, kuhakikisha kura zao zinamwingiza madarakani kwa kishindo mgombea wa urais kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Nyalandu amesisitiza kuwa ushindi wa Dkt. Samia utakuwa chachu ya kuendeleza kasi ya maendeleo yaliyokwisha kuonekana katika sekta mbalimbali, ikiwemo miundombinu, elimu, afya na ustawi wa jamii, huku akiwasihi wananchi wa Kigoma kuwa mstari wa mbele katika kulinda heshima na ushindi wa chama chao

Nyalandu akiwapungia mkono wana CCM baada ya kuwasili mkoani Kigoma kusaka kula za wagombea wa CCM.
Nyalandu akisaini katika kitabu cha wageni baada ya kuwasili mkoani Kigoma kusaka kura.
Wana CCM wa Mkoa wa Kigoma wakionesha furaha yao kufuatia ujio wa Nyalandu mkoani humo wa kuwatafutia kura wagombea wa CCM.
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad