Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan
........................................
Na Mwandishi Wetu
Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema amelipokea na atalifanyia kazi ombi la Mbunge wa Nzega Mjini ambaye pia ni Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe la kuidhinisha kugawanywa kwa Mkoa wa Tabora ili upatikane Mkoa mwingine wa Nzega kwakuwa Mkoa wa Tabora ni mkubwa.
Akiongea leo September 10, 2025 wakati wa kampeni Nzega Mjini, Dkt. Samia amesema ““Yote nayabeba na nakwenda kuyafanyia kazi, na mwenyewe anajua ndio maana kaniambia usijibu hapa lakini yabebe ukayafanyie kazi, kwahiyo la Halmshauri, la Campus ya UDSM kujengwa Nzega, na hili la Mkoa nakwenda kulifanyia kazi kwa undani zaidi”
Akiongea mbele ya Dkt. Samia wakati akitoa ombi hilo, Bashe amesema “Sisi hapa ombi letu kwako Mh. Mgombea, Watu wa Bukene ili aende kwenye makao makuu ya Halmashari ya Nzega Vijijini anasafiri zaidi ya KM 220, Mgombea ombi langu kwako katika kipindi chako cha pili nakuomba Rais tufikirie kuwepo na Halmashauri ya Bukene na Halmshauri ya Ndara, na nakutoa hofu kuhusu uwezo na rasilimali za kuendesha Halmashauri hizo hakuna tatizo”









No comments:
Post a Comment