..................................................
MGOMBEA nafasi ya Ubunge Jimbo la Mbinga Vijijini mkoani Ruvuma, Judith Salvio Kapinga (Malikia wa Mbinga) Leo September 10-2025 amefanya mikutano ya kampeni katika vijiji vya Ukombozi, Mtundualo, Ruanda na Paradiso vilivyopo Kata ya Ruanda katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Kapinga akitoa hotuba yake katika mikutano hiyo, amewaahidi wananchi wa Jimbo la Mbinga vijijini na Kata ya Ruanda kuwa amejipanga vyema kuwatumikia kwa uadilifu na kuisimamia vyema ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM ) ya mwaka 2025/2030.
Aidha, Kapinga ametumia nafasi hiyo kumuombea kura Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amemtaja kuwa ni tumaini na kinara namba moja wa maendeleo ya watanzania na wana Mbinga vijijini, hivyo ikifika Oktoba 29 wananchi wote wajitokeze kwa wingi kwenda kuwapigia kura wagombea wote wanaotokana na CCM ambao ni Diwani, Mbunge na Rais ili waendeleze maendeleo ya kiuchumi, kisiasa, kijamii, kiutamaduni na kitekinolojia.
Kwa upande wake Mgombea udiwani Kata ya Ruanda ya Ruanda kupitia CCM, Deogratias Mwingira naye amewaomba wananchi wa Kata hiyo kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 kuwapigia kura wagombea wanaotokana na CCM.
Taarifa hii imetolewa na Comrade Angelo madundo Mratibu wa timu ya Kampeni-CCM Jimbo la Mbinga vijijini 10/09/2025.










No comments:
Post a Comment