Mratibu wa timu ya kampeni CCM Jimbo la Mbinga Vijijini, Angelo Madundo, akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini katika mkutano wa kampeni uliofanyika Septemba 11, 2025 Kijiji cha Luhagala.
........................
Na Mwandishi Wetu, Mbinga
Mgombea wa ubunge Jimbo la Mbinga vijijini mkoani Ruvuma
Wakili Judith Kapinga ( Malikia wa Mbinga) anaendelea kwa mwendo wa kasi kufanya
mikutano yake ya kampeni kata kwa kata, kijiji kwa kijiji na kuhakikisha Chama Cha
Mapinduzi (CCM), kinaibuka na ushindi
mnono.
Leo September 11-2025 amefanya mikutano ya kampeni Vijiji
vya Luhagala, Mabuni, Litumbandyosi na Kingoli vilivyopo Kata ya Litumbandyosi
katika Halmashauri ya wilaya ya Mbinga.
Katika mikutano hiyo ameendelea kuinadi Ilani ya uchaguzi ya
CCM ya mwaka 2025/2030 na kutaja vipaumbele vyake atakavyovifanyia kazi iwapo
atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Alivitaja vipaumbele hivyo kuwa ni uboreshaji wa huduma za maendeleo
ya jamii kwenye sekta ya maji, afya, Elimu, umeme, miundombinu ya barabara, mawasiliano,
kilimo na usalama wa chakula.
Aidha, Kapinga amewaomba wananchi ifikapo oktoba 29 wajitokeze kwa wingi na
kuwapigia kura wagombea wanaotokana na CCM ili waendelee kuwaletea maendeleo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa timu ya kampeni ya jimbo hilo, John Mkandawile naye amewaomba wananchi wa Kata ya Litumbandyosi na Jimbo la Mbinga vijijini kwa ujumla wake ifikapo oktoba 29 kujitokeza kwa wingi kupiga kura za ndio kwa mgombea nafasi ya urais wa chama hicho Dkt. Samia Suluhu Hassan, mgombea ubunge Judith Kapinga pamoja na mgombea udiwani John Yapalama ili kwa pamoja waweze kuitekeleza ilani ya uchaguzi ya mwaka 2025/2030.
Imetolewa na: CDE Angelo Madundo Mratibu wa timu ya kampeni CCM Jimbo la Mbinga
vijijini 11/09/2025.
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Mbinga Vijijini mkoani Ruvuma Wakili Judith Kapinga ( Malikia wa Mbinga,akihutbia wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika Septemba 11, 2025 Kijiji cha Luahala.











No comments:
Post a Comment