Mgombea Ubunge Jimbo la Kilindi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Salehe Mbwana Mhando (Maarufu kwa jina la Kitochi kushoto) akitambulishwa na Mjumbe wa NEC Mkoa wa Tanga, Mohamed Salim 'RATCO' wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho uliofanyika eneo la Kwediboma mkoani Tanga Septemba 10,2025.
.............................................
Na Mashaka Kibaya, aliyekuwa Kwediboma - Wilayani Kilindi.
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Kilindi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Salehe Mbwana Mhando 'AKA Kitochi', amesema kwamba iwapo wananchi watampatia ridhaa na kuingia madarakani atahangaika usiku na mchana kuchochea harakati za ujenzi wa miundombu ya barabara hatua ambayo itaweza kusaidia kuimarisha uchumi.
Ameyasema hayo Leo (Septemba 10, 2025) kwenye mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni uliofanyika kwenye eneo la Kwediboma Wilayani Kilindi ambapo mgeni rasmi alikuwa mjumbe wa NEC kupitia Mkoa wa Tanga, Mohamed Salim 'RATCO'.
Akizungumza na mamia ya wananchi waliohidhuria mkutano huo, Mhando alisema, anatambua kwamba barabara ndio uhai na maisha ya Wananchi wa Kilindi, hivyo wakimpatia ridhaa suala la ujenzi miundombinu hiyo litakuwa kipaumbele chake.
"Ikifika oktoba 29 msifanye makosa kura nyingi ziwe kwa mgombea wa CCM Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uRais, kura nyingi kwangu na madiwani wa CCM, nitahakikisha kipaumbele changu kinakuwa barabara, mfupa uliokuwa ngumu niachieni Mimi" alisema Mhando akiahidi kushirikiana na Serikali kumaliza changamoto ya barabara.
Aidha Mhando alitanabaisha kuwa wananchi wa Kilindi wanatamani kuona miundombu ya barabara ikifunguka jambo ambalo ndio ajenda iliyopo kwenye mioyo yao ambapo alisema kuwa atahakikisha anafanya ushawishi kwa Serikali ili kumaliza changamoto hiyo .
"Sitolala usiku na mchana kuleta utatuzi miundombinu ya barabara,uzuri ni kuwa yaliyopo kwenye dhamira ndio yapo karika Ilani ,pamoja na hayo barabara ya kuinganisha Kilindi na mkoa lazima iwe ya kiwango cha lami "alisema.
Ujenzi wa barabara hiyo itasaidia kufungua zaidi fursa zai kiuchumi kwa wananchi wa Kilindi ambapo mgombea huyo wa Ubunge alisema, eneo la Kilindi ni lenye ardhi yenye rutuba inayotumiwa na wananchi kuendesha kilimo.
Akionesha msisitizo katika kutafuta suluhu juu ya changamoto hiyo ya barabara, Mhando alisema, ujenzi wa miundombinu hiyo utachochea mzunguko wa soko ambao utaiwezesha Kilindi kuchangia pato la Taifa kupitia kilimo.
Kuhusu suala la Maji, Mhando alisema kwamba, pamoja na jitihada kubwa zilizofanywa na Serikali, iwapo wananchi watatoa ridhaa kwa wagombea wa CCM atahakikisha changamoto iliyopo inakwenda inapata suluhisho la kudumu.
Amesema,Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa na maono makubwa ya ujenzi wa gridi ya maji hivyo Wananchi wakimchagua mgombea huyo wa urais na yeye kuingia bungeni atakwenda kuunga mkono hoja hiyo aliyoieleza kuwa itakuwa ukombozi.
Kuhusu migogoro ya wakulima na wafugaji, Mhando alisema, mara nyingi imekuwa ikijitokeza kutokana na kuvurugwa kwa taratibu ambapo akiingia madarakani atahakikisha watu wanaheshimu taratibu za matumizi bora ya ardhi.
Pamoja na hayo ameahidi kuja na mikakati wa ujirani mwema kwa kuitembelea wilaya ya Mvomelo kuona na kujifunza namna ambavyo waliweza kutatua changamoto zilizohuwu wakulima na wafugaji kwenye eneo lao.
Ametoa pongezi kwa chama cha mapinduzi kwa kumpatia ridhaa ya kupeperusha bendera kuwania wadhifa wa Ubunge wa Jimbo la Kilindi huku akiomba ushirikiano kwa wanabCCM na wananchi kukiwezesha chama tawala kupata ushindi mnono.
Mhando amesema kwamba,ili wilaya ya Kilindi kuweza kupiga hatua za haraka katika maendeleo, ushirikiano mkubwa unahitajika ambapo ameusihi umma kushikamana na kuchagua CCM ili kushika dola.
Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Mkoa wa Tanga, Mohamed Salim almaarufu 'RATCO' ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo aliwaomba wananchi kuendelea kujenga imani na CCM na kukipa kura nyingi ili kuweza kushika dola.
Katika hotuba yake RATCO alisema, mgombea wa ubunge wa Jimbo la Kilindi Salehe Mbwana Mhando ni dira mpya na lulu kwa Wananchi wa Kilindi hivyo hawapaswi kuipoteza akiwasihi kuienzi kwa kura nyinyi zisizo na idadi.
Mgombea Ubunge Jimbo la Kilindi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Salehe Mbwana MhandoUzinduzi ukiendelea.
Taswira ya uzinduzi huo.
Uzinduzi ukiendelea.
Mgombea ubunge huyo akisalimiana na viongozi mbalimbali.









No comments:
Post a Comment